Language 
   

Ujumbe, 25 Agosti 2025

Wanangu wapendwa! Wanangu, wapenzi wangu! Mmechaguliwa kwa sababu mmeitikia, mmeweka maelekezo yangu katika vitendo, na mnampenda Mungu zaidi ya yote. Kwa hiyo, wanangu, ombeni kwa moyo wote ili maneno yangu yapate kutimia. Fungeni, toeni sadaka, pendeni kwa upendo wa Mungu aliyewaumba, na muwe, wanangu, mikono yangu iliyonyooshwa kwa ulimwengu huu ambao haujapata kumjua Mungu wa upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
25 Julai 2025 (Monthly)
25 Septemba 2025 (Monthly)
 
To compare Medjugorje messages with another language versions choose