Our Lady of Medjugorje Messages containing 'amueni'
Total found:
4
Ujumbe, 25 Oktoba 2015
“
W
anangu wapendwa, sala yangu hata leo ni kwa ajili yenu nyote, hasa kwa wale walio na mioyo migumu kuitikia wito wangu. Mnaishi katika siku za neema wala hamtambui fadhili ambazo Mungu anawapeni kwa njia ya uwepo wangu. Wanangu,
amueni
hata leo kuwa watakatifu na jifunzeni kutokana na mifano ya watakatifu wa siku hizi na mtatambua ya kuwa utakatifu ni ukweli uliopo kwa ajili yenu nyote. Wanangu, furahini katika upendo kwa maana machoni pa Mungu ninyi ni wa pekee na hakuna atakayechukua nafasi ya mwingine, kwa maana ninyi ni furaha ya Mungu duniani hapa. Mshuhudieni amani, sala na upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2020
“
W
anangu wapendwa, katika miaka hii yote mimi nipo pamoja nanyi ili kuwaongoza kwenye njia ya wokovu. Rudieni kwa Mwanangu, rudieni katika sala na mfungo. Wanangu, mwachieni Mungu aongee na mioyo yenu kwa sababu shetani anatawala na anatamani kuangamiza maisha yenu na dunia mnamotembelea. Muwe na ujasiri na
amueni
kuwa watakatifu. Mtaona wongofu katika mioyo yenu na katika familia zenu, sala itasikilizwa, Mungu atayapokea maombi yenu na kuwapa amani. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2021
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga na kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani. Huu ni wakati wa mwamko na wa kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji wa amani na wa upendo wenye furaha ili kuishi vizuri duniani. Tamanini Mbingu kwa sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio. Kwa hiyo, wanangu,
amueni
tena kuongoka, na utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2021
“
W
anangu wapendwa! Ninawatazama na kuwaalika: mrudieni Mungu maana Yeye ndiye upendo na kwa ajili ya upendo alinituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya wongofu. Acheni dhambi na maovu,
amueni
kuwa watakatifu na furaha itatawala; nanyi mtakuwa mikono yangu iliyopanuliwa katika ulimwengu huu uliopotea. Ninatamani ya kuwa muwe sala na matumaini kwa wale ambao hawajamjua Mungu wa upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose