Our Lady of Medjugorje Messages containing 'atawabariki'
Total found:
4
Ujumbe, 25 Novemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalika kurudi katika sala. Katika wakati huu wa neema, Mungu amenijalia kuwaongoza kuelekea utakatifu na maisha ya unyofu, ili katika mambo madogo muweze kumtambua Mungu Mwumbaji, kumpenda na ili maisha yenu yawe shukrani kwa Mungu Mkuu kwa yote aliyowajalia. Wanangu, maisha yenu yawe zawadi kwa wengine katika upendo naye Mungu
atawabariki
. Nanyi, mumshuhudie bila kutafuata faida, kwa ajili ya upendo kwa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi nyote mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2018
“
W
anangu wapendwa! Hata viumbe vinawapa ishara za upendo wake Mungu kwa njia ya matunda vinayowapa. Nanyi, pia kupitia ujio wangu, mmepokea wingi wa zawadi na matunda. Wanangu, kadiri mlivyoitikia mwaliko wangu, Mungu anajua. Mimi ninawaalika: hamkuchelewa, kateni shauri kuwa watakatifu na kwa maisha ya pamoja na Mungu katika neema na katika amani! Mungu
atawabariki
na kuwapa mara mia zaidi, ikiwa mnamtumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2019
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali. Sala iwe manukato kwa roho zenu kwani tunda la sala ni furaha, kutoa, kumshuhudia Mungu kwa wengine kwa njia ya maisha yenu. Wanangu, mkimtegemea Mungu kabisa, Yeye atashughulika yote,
atawabariki
na sadaka zenu zitapata maana. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2023
“
W
anangu wapendwa! Aliye Juu ameniruhusu niwe miongoni mwenu, niwaombee, niwe Mama yenu na kimbilio lenu. Ninawaalika wanangu, mrudieni Mungu na kwenye maombi na Mungu
atawabariki
kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose