Our Lady of Medjugorje Messages containing 'awape'
Total found:
6
Ujumbe, 2 Machi 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Naja kwenu kama Mama na ninatamani kuwa kwangu kama Mama mtapata maskani, faraja na mapumziko. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa upendo wangu, salini! Salini kwa moyo mkunjufu, utii na uaminifu kamili kwa Baba wa Mbinguni. Muwe na uaminifu, kama vile mimi pia nilivyokuwa mwaminifu nilipoambiwa ya kuwa nitachukua baraka za ahadi. Basi kutoka mioyo yenu yafike siku zote midomoni mwenu maneno haya "Utakalo lifanyike". Kwa hiyo muwe na uaminifu na salini, ili mimi niweze kuwaombeeni kwa Bwana, ili
awape
Baraka ya Mbinguni na kuwajaza Roho Mtakatifu. Hapo mtaweza kuwasaidia wale wote wasiomjua Bwana. Ninyi, mitume wa upendo wangu, mtawasaidia kumwita "Baba" kwa uaminifu wote. Salini kwa ajili ya wachungaji wenu na mujiaminishe katika mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2018
“
W
anangu wapendwa! Kipindi hiki kiwe kwenu kipindi cha sala ili Roho Mtakatifu, kwa njia ya sala, ashuke juu yenu na
awape
wongofu. Fungueni mioyo yenu na someni Maandiko Matakatifu ili, kwa njia ya ushahidi, ninyi pia muweze kuwa karibu zaidi na Mungu. Wanangu, tafuteni hasa Mungu na vitu vya Mungu na acheni duniani vile vya dunia, maana Shetani huwavuta kwa mavumbi na dhambi. Ninyi mnaalikwa katika njia ya utakatifu na mmeumbwa kwa ajili ya Mbingu. Tafuteni, kwa hiyo, Mbingu na vitu vya mbinguni. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2018
“
W
anangu wapendwa, leo pia ninawaalika kuishi pamoja na Yesu maisha yenu mapya. Bwana Mfufuka
awape
nguvu ili muwe daima mashujaa katika majaribu ya maisha, na waaminifu na mdumu katika kusali, maana Yesu aliwaokoeni kwa majeraha Yake na kwa njia ya Ufufuko Wake aliwapa maisha mapya. Salini, wanangu na msipoteze matumaini. Katika mioyo yenu na ziwe furaha na amani, muwe mashahidi ya furaha ya kuwa wangu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2018
“
W
anangu wapendwa! Hii ni siku ambayo Bwana amenipa kwa kumshukuru kwa kila mmoja wenu, kwa wale walioongoka na waliokubali habari zangu na walioshika njia ya wongofu na ya utakatifu. Wanangu, furahini, maana Mungu ni mwenye rehema na anawapenda wote kwa Upendo wake mkubwa sana na kuwaongoza kuelekea njia ya wokovu kwa msaada wa kuja kwangu hapa. Mimi ninawapenda wote na ninawapa mwanangu ili Yeye
awape
amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2022
“
W
anangu wapendwa! Mungu ananiruhusu niwe pamoja nanyi na kuwaongoza kwenye njia ya amani ili kupitia amani ya kibinafsi, muweze kujenga amani duniani. Nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa Mwanangu Yesu ili
awape
imani thabiti na tumaini ya maisha bora ya baadaye ninayotaka kujenga pamoja nanyi. Ninyi, jipeni moyo na msiogope maana Mungu yu pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana shetani anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili Mungu
awape
amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu wa kisasa hataki Mungu. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu, ni tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira yenu na muwe watu wa amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose