Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kuelekea'
Total found:
23
Ujumbe, 25 Machi 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninasikiliza kilio chenu na maombi ya amani. Shetani amekuwa akipigania vita kwa miaka mingi. Kwa hiyo Mungu amenituma kati yenu ili niwaongoze katika njia ya utakatifu, kwa sababu ubinadamu uko kwenye njia panda. Nawaalikeni: mrudieni Mungu na amri za Mungu mkae vizuri hapa duniani na mtoke katika janga hili ambalo mmeingia kwa sababu humsikii Mungu anayewapenda na anayetaka kuwaokoa na kuwaongoza
kuelekea
maisha mapya. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2023
“
W
anangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata
kuelekea
Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza
kuelekea
furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe
kuelekea
mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2