Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kuongoka'
Total found:
5
Ujumbe, 25 Juni 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo Yeye Aliye Juu ananipa neema ya kuweza kuwapenda na kuwaalika muweze
kuongoka
. Wanangu, Mungu awe kesho yenu, vita, wasiwasi, huzuni yasiwatawale, ila furaha na amani zitawale mioyoni mwa watu wote, na mjue kuwa pasipo Mungu hamtapata kamwe amani. Kwa hiyo, wanangu, mrudieni Mungu na sala ili mioyo yenu iimbe kwa furaha. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawapenda kwa upendo usio na kipimo. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2016
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema nawaalikeni nyote
kuongoka
. Wanangu, mnapenda kidogo, na bado mnasali kidogo. Mmepotea wala hamjui lengo lenu ni nini. Chukueni msalaba wenu, mwangalieni Yesu mumfuate. Yeye anajitoa kwenu hata kufa msalabani maana anawapenda. Wanangu, nawaalikeni kurudia kusali kwa moyo kwa maana katika sala mnaweza kupata matumaini na maana ya uwepo wenu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika kuishi kwa kina imani yenu na kumwomba Aliye juu ili aiimarishe, hivyo upepo na dhoruba yasije yakaivunja. Mizizi ya imani yenu iwe sala na tumaini katika uzima wa milele. Tokea sasa, wanangu, jijengeni wenyewe, katika wakati huu wa neema ambapo Mungu anawapeni neema ili kwa njia ya kujinyima na mwito wa
kuongoka
muwe watu wenye imani na tumaini safi na ya kuvumilia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2017
“
W
anangu wapendwa! Katika kipindi hiki cha neema ninawaalika kusali. Salini na tafuteni amani, wanangu. Yeye aliyekuja hapa duniani awatoe amani, pasipo kuwabagua kuwa ninyi ni nani na ni kitu gani - Yeye, Mwanangu, ndugu yenu, kwa njia yangu anawaalika
kuongoka
maana pasipo Mungu hamna baadaye wala uzima wa milele. Kwa hiyo aminini, salini na isheni katika neema na mkingojea mkutano wenu wa binafsi pamoja naye. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2021
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga na kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani. Huu ni wakati wa mwamko na wa kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji wa amani na wa upendo wenye furaha ili kuishi vizuri duniani. Tamanini Mbingu kwa sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio. Kwa hiyo, wanangu, amueni tena
kuongoka
, na utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose