Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kwa'
Total found:
217
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao Mungu anawajalia
kwa
njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu.
Kwa
hiyo nawaalikeni
kwa
uongofu binafsi na kwenye sala katika familia zenu. Maandiko matakatifu yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote
kwa
baraka yangu ya kimama. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalikeni tena kupenda na kutohukumu. Mwanangu,
kwa
mapenzi ya Baba aliye mbinguni, alikuwapo pamoja nanyi ili awaonyesheni njia ya wokovu, awaokoeni si awahukumuni. Na ikiwa mnataka kumfuata Mwanangu, msihukumu na mpende, kama vile Baba aliye mbinguni anavyowapenda ninyi. Hata wakati mnapoteseka sana, au mnapojikwaa chini ya msalaba, msikate tamaa, msihukumu, bali kumbukeni kwamba mnapendwa, na msifuni Baba aliye mbinguni
kwa
upendo wake. Wanangu, msiiache njia ninayowaongozeni. Msikimbie kwenye maangamizi. Kusali na kufunga itawapa nguvu zaidi ili mweze kuishi kama vile baba wa Mbinguni atakavyo; ili muwe mitume wangu wa imani na upendo; ili maisha yenu iwe na baraka ya wale mnaowaona; ili muwe kitu kimoja na baba aliye mbinguni na Mwanangu. Wanangu, huu ni ukweli wa pekee, ukweli uletao wongofu wenu na kisha wongofu wa wengine wote wasiojua maana ya neno kupenda. Wanangu, Mwanangu aliwapeni wachungaji: muwalinde, na muwaombee. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Mei 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni kuwa na nguvu na imara katika imani na katika sala, ili sala zenu ziwe zenye nguvu za kuweza hata kufungua moyo wa Mwanangu mpendwa Yesu. Salini enyi wanangu wadogo, bila kukoma, ili moyo wenu ujifungue
kwa
upendo wa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi, nawaombea ninyi nyote nikasali
kwa
ajili ya uwongofu wenu. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, katika wakati huu wa wasiwasi nawaalikeni tena kutembea nyuma ya Mwanangu, na kumfuata. Nayajua maumivu, mateso na taabu zenu, lakini katika Mwanangu mtapumzika, ndani yake mtapata amani na wokovu. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu amewakomboa ninyi
kwa
msalaba wake akawajalieni kuwa tena wana wa Mungu na kuwafundisha kumwita tena "Baba" yenu, Mungu aliye mbinguni. Ili muwe wapenzi wa Mungu Baba, basi muwe na mapendo na msamaha,
kwa
kuwa Baba yenu ni upendo na msamaha. Salini na fungeni,
kwa
maana hii ndiyo njia ya kujua na kumfahamu Baba aliye mbinguni. Mtakapomjua huyo Baba, mtafahamu ya kuwa Yeye tu ni muhimu kwenu (Maria Mtakatifu amenena hayo
kwa
nguvu na amkazo sana). Mimi, nikiwa Mama, nataka wanangu wawe watu wenye umoja ambamo Neno la Mungu husikilizwa na kutekelezwa.
Kwa
hiyo, enyi wanangu, mfuateni Mwanangu, muwe kitu kimoja naye, muwe wana wa Mungu. Pendeni wachungaji wenu kama vile Mwanangu alivyowapenda alipowaita kuwatumikia ninyi. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Juni 2013
“
W
anangu wapendwa!
Kwa
furaha moyoni nawapendeni nyote na kuwaalika kuukaribia moyo wangu usio na ndoa, ili moyo wangu uwapeleke karibu zaidi
kwa
Mwanangu, Yesu Kristo, ili naye awajalieni amani yake na upendo wake ambavyo ni chakula
kwa
kila mmoja wenu. Jifungueni, wanangu,
kwa
kusali, na jifungueni
kwa
upendo wangu. Mimi ndimi Mama yenu nisiyeweza kuwaachieni katika mtawanyiko na katika dhambi peke yenu. Enyi wana, mnaalikwa kuwa wanangu, wanangu wapendwa ili niweze kwakabidhi wote
kwa
Mwanangu. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa,
kwa
upendo wa kimama nawaomba mnipe mioyo yenu ili niweze kumtolea Mwanangu, ili naye aweze kuiokoa, kuiokoa kutoka uovu wote unaowafanya daima kuwa watumwa na unaowafanya kuwa mbali na ule Wema wa pekee, yaani Mtoto wangu, anayewaokoa kutoka yote yale yanayowaongoza kwenye njia ya uovu na kuwaondolea amani. Mimi natamani kuwaongoza kwenye uhuru wa ahadi za Mtoto wangu,
kwa
kuwa natamani hapa yatimizwe hasa hasa mapenzi ya Mungu, ili
kwa
kupatanishwa na Baba wa Mbinguni, kufunga na kusali, waweze kuzaliwa mitume wa mapendo ya Mungu, yaani mitume watakaoeneza
kwa
mapendo na uhuru, Mapendo ya Mungu
kwa
watoto wangu wote, mitume watakaoeneza mapendo aminifu
kwa
Baba wa Mbinguni na hivyo kufungua milango ya mbingu. Watoto wapenzi, toeni furaha ya mapendo yenu na mshikamano wenu
kwa
wachungaji wenu kama vile Mtoto wangu alivyowaomba wao kutoa furaha hiyo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Julai 2013
“
W
anangu wapendwa!
Kwa
furaha moyoni nawaalika wote kuishi imani yenu na kuishuhudia
kwa
moyo na mfano
kwa
kila namna. Ee wanangu, kateni shauri kuacha kabisa dhambi na vishawishi vyake; mioyo yenu ijae furaha na upendo
kwa
utakatifu. Mimi, wanangu, nawapenda na ninaambatana nanyi. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, tafadhali muelewe, muwe tayari wote,
kwa
matumaini makuu, kufungua mioyo yenu; hivyo mngeelewa yote, mngeelewa
kwa
upendo gani nawaiteni,
kwa
upendo gani nataka kuwageuza, ili kuwafurahisha,
kwa
upendo gani nataka kuwafanya wafuasi wa Mwanangu na kuwapa amani katika ukamilifu wa Mwanangu. Mngeelewa ukuu wa moyo wangu wa kimama,
kwa
hiyo, wanangu, salini, maana
kwa
njia ya kusali tu imani yenu hukua na upendo wenu huzaliwa, upendo ambao utapunguza uzito wa msalaba
kwa
maana hamtakuwa peke yenu kuubeba. Katika umoja na Mwanangu, tukuzeni jina la Baba wa Mbinguni. Salini, salini mpate tuzo la upendo, maana upendo ni ukweli wa pekee, upendo husamehe yote, hutumikia wote na kuwaona wote kama ndugu. Enyi wanangu, mitume wangu, udhamini ambao Baba wa Mbinguni amewawekeni,
kwa
njia yangu, mtumishi Wake, ni kitu kikubwa, ili kusaidia wale wasiomjua, kusudi zapatanishwe naye, kusudi wamfuate,
kwa
hiyo nawafundisheni kupenda, maana mkiwa na upendo tu mnaweza kumjibu. Nawaalikeni tena: pendeni wachungaji wenu, salini ili katika wakati huu wa shida jina la Mwanangu atukuzwe
kwa
njia ya mwongozo wao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo pia Yeye Aliye Juu anijalia neema ya kuwa pamoja nanyi na kuwaongoza mpate kutubu. Siku hata siku Mimi napanda mbegu na kuwaalika kutubu ili muweze kuwa sala, amani, upendo na ngano ambayo ikifa huzaa mara mia. Sipendi, wanangu wapendwa, mpate kujuta
kwa
yote mliyoweza kufanya wala hamkufanya.
Kwa
hiyo, enyi wanangu, tena
kwa
moyo wa furaha semeni: “ Nataka kuwa ishara
kwa
watu wengine”. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawapendeni, ninyi nyote, watoto wangu nyote, muwe wote moyoni mwangu, ninyi nyote mmepata upendo wangu wa kimama na ninatamani kuwaongoza nyote ili mjue furaha ya Mungu.
Kwa
hiyo nawaalikeni: nahitaji mitume wanyenyekevu ambao,
kwa
moyo mkunjufu, wanapokea Neno la Mungu na ambao wako tayari kuwasaidia watu wengine ili,
kwa
njia ya Neno la Mungu, waelewe maana ya maisha yao. Ili muweze kufanya hayo, wanangu, yawapasa,
kwa
njia ya kusali na kufunga, kusikiliza
kwa
moyo mkunjufu na kujifunza kujidhili au kujinyenyekesha. Yawapasa kujifunza kukataa yote yanayowatenganisha na Neno la Mungu na kutamani tu yanayowakaribisha. Msiogope, mimi nipo hapa. Ninyi si peke yenu. Namwomba Roho Mtakatifu ili awafanye wapya, ili awaimarishe. Namwomba Roho Mtakatifu, ili mkisaidia wengine, muweze kujiponya nyinyi wenyewe. Naomba ili,
kwa
njia yake, muwe wana wa Mungu na mitume wangu.
”
Kisha
kwa
mahangaiko makubwa Bikira Maria alisema:
“
Kwa
ajili ya Yesu,
kwa
ajili ya mwanangu, pendeni wale ambao Yeye aliwaita mkitamani baraka ya mikono ile ambayo Yeye tu ameyaweka wakfu. Msiyaruhusu maovu yatawale. Nawaalikeni tena: ni
kwa
njia ya wachungaji wangu tu moyo wangu utashinda. Msiyaruhusu maovu yawatenganisheni na wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalikeni kusali. Uhusiano wenu na kusali uwe wa kila siku. Sala inasababisha miujiza ndani yenu na
kwa
njia yenu, na
kwa
hiyo, enyi wanangu, sala basi iwe ni furaha yenu. Hivyo uhusiano wenu na maisha utakuwa wa kina na wazi zaidi, pia mtaelewa kwamba maisha ni zawadi
kwa
kila mmoja wenu. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa! nawapendeni
kwa
upendo wa kimama, na
kwa
subira ya kimama nangojea upendo wenu na ushirikiano wenu. Nasali ili muwe jumuiya ya wana wa Mungu na wanangu. Nasali ili muweze kuwa jumuiya inayojihuisha
kwa
furaha na imani na upendo wa Mwanangu. Wanangu, nawakusanya kama mitume wangu na nitawafundisha jinsi ya kuwajulisha wengine upendo wa Mwanangu, na jinsi ya kuwafikishia habari njema, ambaye ni Mwanangu. Nipeni mioyo yenu iliyo wazi na iliyosafishwa, nami nitaijaza upendo wa Mwanangu. Upendo wake utaipa maisha yenu maana nami nitatembea pamoja nanyi. Nitakuwa pamoja nanyi hata tumfikie Baba wa Mbinguni. Wanangu, wataokoka tu wale ambao watatembea
kwa
upendo na imani kumwelekea Baba wa Mbinguni. Msiogope, nipo pamoja nanyi! Muwaamini wachungaji wenu kama Mwanangu alivyowaamini wakati alipowachagua, na muwaombee ili waweze kupata nguvu na upendo wa kuwaongozeni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni mjifungulie
kwa
sali. Sala itasababisha miujiza ndani yenu na
kwa
njia yenu.
Kwa
hiyo, enyi wanangu,
kwa
moyo mkunjufu mtafuteni Yeye Aliye Juu ili awapeni nguvu ya kuwa wana wa Mungu, na yule Shetani asiwatikiseni kama matawi yatikiswavyo na upepo. Kateni shauri tena, wanangu,
kwa
Mungu na tafuteni tu mapenzi yake, hapo mtapata furaha na amani. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa,
kwa
moyo wa kimama nawaalikeni tena kupenda, kusali bila kukata tamaa
kwa
zawadi ya upendo, kumpenda Baba wa Mbinguni zaidi ya yote. Mtakapompenda Yeye, mtajipenda wenyewe na jirani zenu. Mambo hayo hayawezi kutengana. Baba wa Mbinguni yumo katika kila mtu, hupenda kila mtu na kumwita kila mtu
kwa
jina lake.
Kwa
hiyo, wanangu,
kwa
njia ya kusali sikilizeni atakalo Baba wa Mbinguni. Ongeeni na Yeye. Muwe na uhusiano wa binafsi pamoja na Baba, atakayeufanya mkubwa zaidi uhusiano wake nanyi, jumuhiya ya wanangu, mitume wangu. Kama Mama napenda kwamba,
kwa
njia ya upendo kumwelekea Baba wa Mbinguni, inukeni juu ya ubatili wa malimwengu na muwasaidie wengine kujua na kumjongea polepole Baba wa Mbinguni. Wanangu, salini, salini, salini
kwa
zawadi ya upendo,
kwa
sababu upendo ndiye Mwanangu. Muwaombee wachungaji wenu, ili wawapende ninyi siku zote, kama vile Mwanangu alivyowapenda ninyi na kuonyesha akitoa maisha yake
kwa
wokovu wenu. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni nyote kusali. Fungueni
kwa
kina mlango wa mioyo yenu, enyi wanangu,
kwa
sala, sala ya moyo na hivyo Yeye Aliye Juu ataweza kufanya kazi katika uhuru wenu na kuanzisha uongofu wenu. Hivyo imani yenu itakuwa imara kiasi cha kuweza kusema
kwa
moyo wenu wote: "Mungu wangu na yote yangu". Halafu mtaweza kuelewa, wanangu, ya kuwa duniani hapa yote hupita. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa,
kwa
upendo wa kimama na uvumilivu wa kimama naona kutangatanga kwenu na kuendelea kupotea kwenu.
Kwa
sababu hiyo mimi nipo pamoja nanyi. Nataka kwanza kabisa kuwasaidieni kupata kujijua ninyi wenyewe, ili baadaye muweze kuelewa na kutambua yote yanayowazuia kujua bila unafiki na
kwa
moyo wote upendo wa Baba wa Mbinguni. Wanangu, Baba hujulikana
kwa
njia ya msalaba:
kwa
hiyo msikatae msalaba:
kwa
msaada wangu, mkafanye bidii kuuelewa na kuupokea. Mtakapoweza kuupokea msalaba, mtaelewa pia upendo wa Baba wa Mbinguni. Mtatembea pamoja na Mwanangu na mimi. Mtajipambanua na wale ambao hawakujua upendo wa Baba wa Mbinguni, kujitofautisha na wale wanaomsikiliza lakini hawamwelewi, na wale wasioenda pamoja naye, na wasiomjua. Mimi nataka ninyi mjue ukweli wa Mwanangu na muwe mitume wangu; ili, kama wana wa Mungu, muwe na mawazo yaliyo juu ya mawazo ya kibinadamu na siku zote na katika yote mkatafute kila mara mawazo ya Mungu. Wanangu, salini na fungeni ili muweze kuelewa yote ninayowaombeni. Muombee wachungaji wenu mkatamani kujua, mkishirikiana nao, upendo wa Baba wa Mbinguni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mfalme wa amani ili Yeye awapatie amani Yake. Ninyi, wanangu, salini, salini, salini. Matunda ya sala yatajionyesha kwenye nyuso za watu waliojitoa
kwa
Mungu na Ufalme wake. Mimi pamoja na mwanangu Yesu tunawabariki nyote
kwa
baraka ya amani. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Ili mpate kuwa mitume wangu na kuweza kusaidia wale walioko katika giza, ili waweze kuujua mwanga wa upendo wa Mwanangu, mnapaswa kuwa na moyo safi na mnyenyekevu. Hamwezi kusaidia ili Mwanangu azaliwe na kutawala mioyoni mwa wale wasiomjua, iwapo Yeye hatawali moyoni mwenu. Mimi nipo pamoja nanyi, natembea pamoja nanyi kama mama, nabisha hodi katika moyo wenu, usioweza kufunguka bila ya kuwa mnyenyekevu. Mimi nasali, lakini salini nanyi pia, wanangu wapendwa, ili muweze kumfungulia Mwanangu moyo wenu safi na mnyenyekevu na hivyo kuweza kupokea vipaji nilivyowaahidi. Hapo ndipo mtakapoongozwa
kwa
upendo na nguvu za Mwanangu, hapo ndipo mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza
kwa
walio karibu yao matunda ya upendo wa Mungu. Kutokana na ninyi na
kwa
njia yenu Mwanangu atafanya kazi, maana mtakuwa na Yeye kitu kimoja. Moyo wangu wa kimama unatamani muungano wa wanangu wote,
kwa
njia ya Mwanangu.
Kwa
upendo mkuu nawabariki na kuwaombea wateule wa Mwanangu, wachungaji wenu, Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, salini ili mionzi ya sala yenu iwaguse watu wote mnaokutana nao. Wekeni Biblia Takatifu mahali pa kuonekana katika familia zenu, mkaisome ili maneno ya amani yatiririke ndani ya mioyo yenu. Nasali pamoja nanyi na
kwa
ajili yenu, wanangu, ili siku hata siku mzidi kuyapokea mapenzi ya Mungu. Asanteni
kwa
kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa!
Kwa
upendo wa kimama nataka kuwafundisha uadilifu, natamani kwamba katika kutenda kwenu kazi kama mitume wangu muwe wenye haki, maamuzi na hasa waadilifu. Natamani kwamba,
kwa
neema ya Mungu, muweze kupokea Baraka ya Mungu. Natamani,
kwa
njia ya kufunga na kusali, muweze kupata kutoka
kwa
Baba wa Mbinguni ujuzi, uhalali, utakatifu wa kimungu.
Kwa
ulinzi wa Mwanangu na wangu mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza neno la Mungu
kwa
wote wasiolijua, na mtaweza kushinda mapingamizi mtakayokutana nayo njiani. Wanangu,
kwa
njia ya baraka neema itawashukia, nanyi mtaweza kuilinda neema hiyo
kwa
kufunga na kusali,
kwa
kujitakasa na kujipatanisha. Mtakuwa na utendaji fanisi ninaohitaji kutoka kwenu. Waombeeni wachungaji wenu ili mionzi ya neema ya Mungu iangaze njia yao. Nawashukuru.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>