Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mpango'
Total found:
5
Ujumbe, 25 Julai 2014
“
W
anangu wapendwa! Ninyi hamjui neema ya namna gani mnayoishi katika wakati huu ambapo Yeye Aliye Juu awapeni ishara ili mjifungue na kutubu. Mwelekeeni Mungu na kusali; sala itawale katika mioyo yenu, familia na jamaa zenu ili Roho Mtakatifu awaongoze na kuhimiza kila siku mjifungue kufanya mapenzi ya Mungu na
mpango
wake kwa kila mmoja wenu. Mimi nipo pamoja nanyi, na nawaombeeni pamoja na malaika na watakatifu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini kwa nia zangu maana Shetani ataka kuangamiza
mpango
wangu nilio nao hapa na kuwaibia amani: Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini ili Mungu aweze kutenda kazi kwa njia ya kila mmoja wenu. Mioyo yenu iwe wazi kupokea mapenzi ya Mungu. Mimi nawapendeni na kubariki kwa baraka ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Machi 2018
“
W
anangu wapendwa, ninawaalika kukaa pamoja nami katika kusali, wakati huu wa neema, ambapo giza linapigana na mwagaza. Wanangu, salini, muungame dhambi zenu mkaanzishe maisha mapya katika neema. Kateni shauri kwa Mungu naye atawaongoza kuelekea utakatifu na msalaba utakuwa kwenu ishara ya ushindi na matumaini. Mjivunie kubatizwa na mshukuruni moyoni mwenu kushika
mpango
wa Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2019
“
W
anangu wapendwa, Mungu kwa rehema yake alinijalia kuwa pamoja nanyi, ili kuwaelimisha na kuwaongoza kuelekea katika hatua ya wongofu. Wanangu, ninyi nyote mmeitwa kusali kwa moyo wenu wote ili
mpango
wa wokovu utimilike ndani mwenu na kwa njia yenu. Jueni wanangu, kwamba maisha ni mafupi na uzima wa milele unawangoja kwa kadiri ya mastahili yenu. Kwa hiyo salini, salini, salini ili muweze kuwa vyombo vya kufaa mikononi mwa Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2022
“
W
anangu wapendwa! Ninafurahi pamoja nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa makusudi yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika
mpango
wangu wa wokovu wa wanadamu. Rudeni kwa Mungu na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu, Mimi ni pamoja nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose