Our Lady of Medjugorje Messages containing 'mwumbaji'
Total found:
4
Ujumbe, 25 Aprili 2016
“
W
anangu wapendwa! Moyo wangu usio na doa unatoka damu nikiwaangalieni katika dhambi na mazoea mabaya. Nawaalika: mrudieni Mungu na salini ili mpate kufanikiwa duniani. Mungu anawaalika kwa njia yangu ili mioyo yenu iwe tumaini na furaha kwa wale wote walio mbali. Ombi langu liwe kwenu manukato kwa nafsi na moyo ili mtukuze Mungu
Mwumbaji
anayewapenda na kuwaalika kwa mambo ya milele. Wanangu, maisha ni mafupi, mtumie nafasi hii kwa ajili ya kutenda mema. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalika kurudi katika sala. Katika wakati huu wa neema, Mungu amenijalia kuwaongoza kuelekea utakatifu na maisha ya unyofu, ili katika mambo madogo muweze kumtambua Mungu
Mwumbaji
, kumpenda na ili maisha yenu yawe shukrani kwa Mungu Mkuu kwa yote aliyowajalia. Wanangu, maisha yenu yawe zawadi kwa wengine katika upendo naye Mungu atawabariki. Nanyi, mumshuhudie bila kutafuata faida, kwa ajili ya upendo kwa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi nyote mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Juni 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nataka kuwashukuru kwa uvumilivu wenu na kuwaalika kujifungua kwa sala ya ndani. Wanangu, sala ni moyo wa imani na wa matumaini katika uzima wa milele. Kwa hiyo salini kwa moyo mpaka moyo wenu umwimbie Mungu
Mwumbaji
aliyewapa maisha kwa shukrani. Wanangu, Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaletea baraka yangu ya amani ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2020
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali tena zaidi ili msikie katika mioyo yenu utakatifu wa msamaha. Katika familia lazima kuwepo utakatifu kwa sababu enyi wanangu, ulimwengu hauna wakati ujao bila upendo na utakatifu, kwa sababu katika utakatifu na katika furaha ninyi mjitolee kwa Mungu
Mwumbaji
anayewapendeni kwa upendo mkubwa sana. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose