Our Lady of Medjugorje Messages containing 'na'
Total found:
216
Ujumbe, 25 Januari 2019
“
W
anangu wapendwa! kama mama ninawaalika kutubu. Wakati huu ni kwenu, wanangu, wakati wa ukimya
na
sala. Kwa hiyo, katika joto la moyo wenu iote chembe ya tumaini
na
imani
na
hivyo, ninyi nanyi, wanangu, siku kwa siku mtasikia haja ya kusali zaidi. Maisha yenu yatakuwa ya mpangilio
na
yenye kuwajibika. Mtaelewa, wanangu, ya kuwa sisi ni wa kupita hapa duniani
na
ya kuwa mtasikia haja ya kuwa karibu zaidi
na
Mungu
na
kwa upendo mtatoa ushuhuda wa mang'amuzi yenu ya kukutana
na
Mungu, mtakaoushirikisha pamoja
na
wengine. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawaombeeni, lakini siwezi kufanya hivyo bila 'Ndiyo' yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, upendo
na
wema wa Baba wa mbinguni yanatoa mafunuo ili kwamba imani ikue, iweze kuelezwa, ilete amani, salama
na
matumaini. Hivi mimi nami, wanangu, kwa ajili ya upendo wenye rehema wa Baba wa mbinguni ninawaonyesha sikuzote tena njia ya kwenda kwa Mwanangu, kwa wokovu wa milele; kwa bahati mbaya, lakini, wanangu wengi hawataki kunisikiliza. Wanangu wengi wanasita. Lakini mimi, mimi, katika wakati
na
zaidi ya wakati, sikuzote nimemtukuza Bwana kwa mambo yale yote aliyoyatenda ndani yangu
na
kwa njia yangu. Mwanangu anajitolea kwenu, anamega mkate pamoja nanyi, anawaambieni maneno ya uzima wa milele ili muweze kuwaletea watu wote. Nanyi, wanangu, mitume wa upendo wangu, mnaogopa nini, ikiwa Mwanangu ni pamoja nanyi? Mwonyesheni nafsi zenu, ili Yeye aweze kuwa ndani yao
na
aweze kuwafanyeni kuwa vyombo vya imani, vyombo vya upendo. Wanangu, ishini Injili, ishini upendo wenye rehema kuelekea mwenzenu; lakini hasa ishini upendo kuelekea Baba wa mbinguni. Wanangu, hamkuungana kwa bahati tu. Baba wa mbinguni haunganishi watu kwa bahati tu. Mwanangu anaongea
na
nafsi zenu, nami ninaongea moyoni mwenu. Kama Mama ninawaambia: tembeeni nami! Pendaneni,
na
kutoa shuhuda! Hampasi kuogopa kulinda Ukweli, ambao ni Neno la Mungu, lililo la milele
na
lisilogeuka kamwe, kwa mifano yenu. Wanangu, yule anayetenda kazi katika mwanga wa upendo wenye rehema
na
ukweli, anasaidiwa sikuzote
na
Mbingu
na
hayuko peke yake. Mitume wa upendo wangu, waweze kuwatambua sikuzote katikati ya wengine wote katika maficho, upendo
na
utulivu wenu. Mimi nipo pamoja nanyi. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2019
“
W
anangu wapendwa! Leo ninawaalika kwa maisha mapya. Haijalishi miaka yenu ni mingapi, fumbueni mioyo yenu kwa Yesu ambaye atawabadilisha katika wakati huu wa neema nanyi, kama nyasi, mtazaliwa katika maisha mapya katika upendo wa Mungu
na
mtafumbua mioyo yenu kwa Mbinguni
na
kwa vitu vya kimbingu. Mimi nipo bado pamoja nanyi maana Mungu aliniruhusu kwa ajili yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, ninawaita mitume wa upendo wangu. Ninawaonyesha Mwanangu, aliye amani ya kweli
na
upendo wa kweli. Kama Mama, kwa ajili ya neema ya kimungu, ninatamani kuwaongoza kwendea Yeye. Wanangu, kwa hiyo ninawaalika kujitazama ninyi wenyewe mkianzia kwa Mwanangu, kumtazama kwa moyo
na
kuona kwa moyo mahali mlipo
na
maisha yenu yanakwenda wapi. Wanangu, ninawaalika kuelewa ya kuwa mnaishi kwa ajili ya Mwanangu, kwa njia ya upendo wake
na
sadaka yake. Ninyi mnamwomba Mwanangu kuwa mwenye rehema nanyi, lakini mimi ninawaalika ninyi kuwa
na
rehema. Mnamwomba kuwa mwema nanyi
na
kuwasamehe, lakini tangu lini mimi ninawasihi ninyi, wanangu, kusamehe
na
kupenda watu wote mnaokutana nao! Mtakapoelewa kwa moyo maneno yangu, mtaelewa
na
kujua upendo wa kweli,
na
mtaweza kuwa mitume wa upendo ule, enyi mitume wangu, wanangu wapendwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2019
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema. Kama vile maumbile huhuisha kwa maisha mapya nanyi pia mnaalikwa kugeuka. Kateni shauri kwa ajili ya Mungu. Wanangu, ninyi ni watupu wala hamna furaha maana hamko
na
Mungu. Kwa hiyo salini ili sala iwe maisha kwenu. Maporini mtafuteni Mungu aliyewaumbeni maana mapori ya asili yanaongea
na
kupigana kwa ajili ya maisha wala si kwa ajili ya kifo. Vita vinatawala katika mioyo yenu
na
katika watu maana hamna amani
na
wala hamuoni, wanangu, ndugu yenu ndani ya jirani yako. Kwa hiyo mrudieni Mungu
na
kusali. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Aprili 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kama Mama ambaye anajua wana wake, ninajua ya kuwa mnamtamani Mwanangu. Ninajua ya kuwa mnatamani ukweli, amani,
na
kilicho chema wala si uovu. Kwa sababu hiyo mimi, kama Mama, kwa njia ya upendo wa Mungu ninawaita ninyi
na
kuwaalika ili, mkisali kwa moyo safi
na
wazi, mmtambue ninyi wenyewe Mwanangu, upendo wake,
na
Moyo wake wenye rehema. Mwanangu alikuwa akiona uzuri katika vitu vyote. Yeye anatafuta mema, hata yale mema madogo yanayofichika, katika roho zote, ili kusamehe maovu. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa upendo wangu, ninawaalika kumwabudu, kumshukuru daima
na
kumstahili. Maana yeye aliwaambieni maneno ya kimungu, maneno ya Mungu, maneno yaliyo kwa watu wote
na
hata milele. Kwa hiyo, wanangu, ishini uchangamfu, umakini, umoja
na
muwe
na
mapenzi baina yenu. Haya mnapaswa kuwa nayo katika ulimwengu wa leo: hivyo mtakuwa mitume wa upendo wangu, hivyo mtashuhudia Mwanangu kwa jinsi ya haki. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2019
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema, wakati wa rehema kwa kila mmoja wenu. Wanangu, msiruhusu upepo wa chukio
na
hofu utawale ndani yenu
na
karibu nanyi. Ninyi, wanangu, mmealikwa kuwa upendo
na
sala. Ibilisi ataka hofu
na
fujo lakini ninyi, wanangu, muwe furaha ya Yesu Mfufuka ambaye amekufa
na
kufufuka kwa ajili ya kila mmoja wenu. Yeye ameshinda kifo kwa kuwapeni uzima, uzima wa milele. Kwa hiyo, wanangu, mshuhudieni
na
muwe wenye fahari kwa kufufuliwa katika Yeye. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama ninawaalika ili kwa moyo safi
na
wazi, kwa imani kabisa, mpokee upendo mkubwa wa Mwanangu. Mimi ninajua ukuu wa upendo wake, mimi nilimchukua ndani yangu, Hostia moyoni, Mwanga
na
Upendo wa ulimwengu. Wanangu, hata kuelekea kwangu kwenu ninyi ni ishara ya upendo
na
ya huruma ya Baba wa Mbinguni, ni tabasamu kilichojaa upendo wa Mwanangu, ni mwaliko kwa uzima wa milele. Damu ya Mwanangu ilimwagika kwa ajili yenu kwa upendo. Ile Damu yenye thamani ni kwa wokovu wenu, kwa ajili ya uzima wa milele. Baba wa mbinguni aliumba mtu kwa ajili ya furaha ya milele. Haiwezekani ninyi kufa, ninyi mnaojua upendo wa Mwanangu, ninyi mnaomfuata. Uzima umeshinda: Mwanangu yu hai! Kwa hiyo, wanangu, mitume wa upendo wangu, sala iwaonyeshe njia, jinsi ya kueneza upendo wa Mwanangu kwa jinsi ilivyo bora zaidi. Wanangu, hata wakati mnapojaribu kuishi maneno ya Mwanangu, ninyi mnasali. Wakati mnapowapenda watu mnaokutana nao, mnaeneza upendo wa Mwanangu. Upendo ni neno linalofungua milango ya Uzima. Wanangu, tangu awali nimesali kwa ajili ya Kanisa. Kwa hiyo ninawaalika nanyi, mitume wa upendo wangu, kusali kwa ajili ya Kanisa
na
watumishi wake, kwa wale ambao Mwanangu amewaita. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Mei 2019
“
W
anangu wapendwa, Mungu kwa rehema yake alinijalia kuwa pamoja nanyi, ili kuwaelimisha
na
kuwaongoza kuelekea katika hatua ya wongofu. Wanangu, ninyi nyote mmeitwa kusali kwa moyo wenu wote ili mpango wa wokovu utimilike ndani mwenu
na
kwa njia yenu. Jueni wanangu, kwamba maisha ni mafupi
na
uzima wa milele unawangoja kwa kadiri ya mastahili yenu. Kwa hiyo salini, salini, salini ili muweze kuwa vyombo vya kufaa mikononi mwa Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, moyo safi
na
wazi tu utawawezesha ninyi kumjua kweli Mwanangu,
na
wale wote wasiojua upendo wake kuujua kwa njia yenu. Upendo tu utawawezesha kuelewa kuwa ni wenye nguvu kuliko kifo, maana upendo wa kweli umeshinda kifo
na
umefanya hata kifo hakipo tena. Wanangu, msamaha ni mtindo bora wa upendo. Ninyi, kama mitume wa upendo wangu, yawapasa kusali kwa kuwa wenye nguvu katika roho
na
kuweza kuelewa
na
kusamehe. Ninyi, mitume wa upendo wangu, kwa njia ya ufahamu
na
msamaha, mnatoa mfano wa upendo
na
rehema. Kuweza kuelewa
na
kusamehe ni karama inayotokana
na
maombi
na
yatupasa kuitunza. Mkisamehe ninyi mnaonyesha ya kuwa mnajua kupenda. Tazameni, wanangu, kama Baba wa mbinguni anavyowapenda kwa upendo mkubwa, kwa ufahamu, kwa uelewa, msamaha
na
haki. Kama anavyowatolea mimi, Mama wa mioyo yenu.
Na
tazama: mimi nipo katikati yenu ili kuwabariki kwa baraka ya kimama; ili kuwaalika kusali
na
kufunga; ili kuwasihi kuamini, kutumaini, kusamehe, kuwaombea wachungaji wenu
na
hasa kupenda bila mipaka. Wanangu, nifuateni! Njia yangu ni njia ya amani
na
upendo, njia ya Mwanangu. Ndiyo njia ya kuongoza katika ushindi wa Moyo wangu. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Juni 2019
“
W
anangu wapendwa, Namshukuru Mungu kwa kila mmoja wenu. Hasa, wanangu, asanteni kwa kuitikia wito wangu. Mimi ninawatayarisha kwa nyakati mpya ili muwe imara katika imani
na
kusali daima, ili Roho Mtakatifu atende kwa njia yenu
na
afanye upya uso wa nchi. Ninasali pamoja nanyi kwa amani, karama ya thamani kuliko zote, hata ingawa shetani hutaka vita
na
machukio. Ninyi, wanangu, muwe mikono yangu inayonyoshwa
na
tembeeni katika kujivunia pamoja
na
Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Julai 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kufuatana
na
matakwa ya Baba mwenye rehema, nimewapa
na
tena nitawapa ishara dhahiri za uwepo wangu wa kimama. Wanangu, ishara hizo ni kwa hamu yangu ya kimama ya kuziponya roho. Ishara hizo ni kwa hamu ya kuwa kila mwanangu awe
na
imani ya kweli, aishi mang’amuzi ya ajabu akinywa kwenye chemchemi ya Neno la Mwanangu, Neno la uhai. Wanangu, kwa njia ya upendo wake
na
sadaka, Mwanangu alichukua ulimwenguni mwanga wa imani
na
aliwaonyesheni njia ya imani. Maana, wanangu, imani huamsha huzuni
na
maumivu. Imani ya kweli hufanya sala kusisika zaidi, hutimiza matendo ya huruma: mazungumzo
na
matoleo. Wale wanangu walio
na
imani, imani ya kweli, ni wenye heri pamoja
na
yote, maana wanaishi duniani mwanzo wa heri ya Mbinguni. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa upendo wangu, ninawaalika kutoa mfano wa imani ya kweli, kupeleka mwanga pale palipo giza, kumwishi Mwanangu. Wanangu, kama Mama ninawaambia: hamwezi kupitia njia ya imani
na
kumfuata Mwanangu pasipo wachungaji wenu. Salini ili wawe
na
nguvu
na
upendo kwa kuwaongoza. Sala zenu ziwe sikuzote pamoja nao. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Julai 2019
“
W
anangu wapendwa, mwaliko wangu kwenu ni sala. Sala iwe kwenu furaha
na
taji la kuwaunganisha
na
Mungu. Wanangu, majaribu yatakuja nanyi hamtakuwa
na
nguvu
na
dhambi itatawala lakini mkiwa wangu, mtashinda maana kimbilio lenu litakuwa Moyo wa Mwanangu Yesu. Kwa hiyo wanangu, rudieni sala ili sala iwe maisha kwenu, mchana
na
usiku. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Upendo wa Mwanangu ni mkubwa. Laiti mngeweza kujua ukuu wa upendo Wake, msingeacha kamwe kumwabudu
na
kumshukuru. Yeye ni sikuzote hai pamoja nanyi katika Ekaristi, maana Ekaristi ni moyo Wake, Ekaristi ni moyo wa imani. Yeye hakuwaacha kamwe: hata wakati ninyi mlipojaribu kwenda mbali Naye, Yeye hakuwaacha kamwe.
Kwa hiyo, moyo wangu wa kimama unafurahi wakati unapotazama jinsi mlivyojaa upendo mnapomrudia, wakati unapoona ya kuwa mnamrudia kwa njia ya upatanisho, upendo
na
matumaini. Moyo wangu wa kimama unajua ya kuwa ikiwa mngetembea katika njia ya imani, mngekuwa kama machipukizi, kama matumba
na
kwa njia ya sala
na
kufunga mngekuwa kama matunda, kama maua, mitume wa upendo wangu, mngekuwa waleta mwanga
na
mngeangaza kwa upendo
na
hekima pande zote karibu nanyi.
Wanangu, kama mama, ninawaomba: salini, fikirini
na
kutafakari. Yote yanayowatokea, mazuri, ya kuumiza
na
ya kufurahisha, hayo yote yawasababisha kukua kiroho, yawafanya kuwa Mwanangu akue ndani yenu. Wanangu mkabidhi kwake. Mumwamini
na
mtumainie upendo Wake.
Na
Yeye awaongoze.
Na
Ekaristi iwe mahali mtakapolisha roho zenu ili kueneza upendo
na
ukweli. Shuhudieni Mwanangu. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2019
“
W
anangu wapendwa, Fanyeni kazi
na
shuhudieni kwa upendo Ufalme wa Mbinguni ili muweze kuwa hamjambo hapa duniani. Wanangu, Mungu atabariki mara mia zaidi juhudi yenu
na
mtakuwa mashahidi katikati ya watu, roho za wale wasioamini zitahisi neema ya wongofu
na
Mbingu itazipokea taabu zenu
na
sadaka zenu. Wanangu, shuhudieni kwa tasbihi mkononi ili muwe wangu
na
kateni shauri kuwa watakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Salini kila siku Tasbihi, taji lile la maua linaloniungana moja kwa moja kama Mama kwa maumivu yenu, mateso, mahitaji
na
matumaini. Mitume wa upendo wangu, Mimi nipo pamoja nanyi kwa njia ya neema
na
upendo wa Mwanangu, nanyi ninawaombeni sala. Sala zenu zinahitajika sana ulimwenguni, ili roho ziongoke! Fungueni wazi kwa imani timilifu mioyo yenu kwa Mwanangu,
na
yeye ataandika ndani yao muhtasari wa Neno lake, yaani upendo. Ishini muungano usiotenganika
na
Moyo Mtakatifu sana wa Mwanangu! Wanangu, kama Mama nawaambieni ya kwamba hakuna wakati wa kupoteza ili kupiga magoti mbele ya Mwanangu, kumkiri kama Mungu wenu, aliye kitovu cha maisha yenu. Mtoeni karama, zile anazozipenda zaidi, yaani upendo kwa jirani yako, rehema
na
mioyo safi. Mitume wa upendo wangu, wanangu wengi bado hawajamkiri Mwanangu kama Mungu wao, bado hawajajua upendo wake. Lakini ninyi, kwa njia ya sala yenu inayosema kwa moyo safi
na
wazi, pamoja
na
karama mnazotoa kwa Mwanangu, mtasababisha kwamba hata mioyo migumu zaidi ifunguke. Mitume wa upendo wangu, nguvu ya sala inayosemwa kutokana
na
moyo, ya sala yenye nguvu
na
iliyojaa upendo, hugeuza ulimwengu. Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini! Mimi nipo pamoja nanyi.. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2019
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali kwa ajili ya makusudi yangu ili niweze kuwasaidia. Wanangu, salini Rosari mkitafakari mafumbo ya Rosari maana hata ninyi katika maisha yenu mnapitia furaha
na
maumivu. Kwa njia hii mtageuza mafumbo katika maisha yenu maana maisha ni fumbo hadi mtakapoyaweka katika mikono ya Mungu. Hivyo mtakuwa
na
mang'amuzi ya imani kama Petro aliyemkuta Yesu
na
Roho Mtakatifu aliyoijaza roho yake. Hata ninyi, wanangu, mnaalikwa kushuhudia mkiishi upendo ambao kwao siku kwa siku Mungu anawajaza kwa njia ya uwepo wangu. Kwa hiyo, wanangu, muwe wazi
na
salini kwa moyo katika imani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, mapenzi
na
upendo wa Baba wa mbinguni hufanya mimi niwe katikati yenu, ili kusaidia kwa upendo wa kimama ukuaji wa imani katika mioyo yenu, ili kwamba muweze hakika kuelewa lengo la maisha ya kidunia
na
ukuu wa yale ya kimbingu. Wanangu, maisha ya kidunia ndiyo njia kuelekea umilele, kuelekea ukweli
na
uzima: kuelekea kwa Mwanangu. Kwa njia hii nataka kuwaongoza. Ninyi, wanangu, ninyi wenye sikuzote kiu ya upendo mkubwa zaidi, ukweli
na
imani, mjue ya kuwa moja tu ni chemchemi mnakoweza kunywa: imani katika Baba wa mbinguni, imani katika upendo wake. Mtegemee kabisa mapenzi yake wala msiogope: kila lililo bora kwa ajili yenu, kila linalowachukua kwenye uzima wa milele, mtapewa! Mtaelewa ya kuwa lengo la maisha si sikuzote kutaka
na
kutwaa, lakini kupenda
na
kutoa; mtakuwa
na
amani ya kweli
na
upendo wa kweli, mtakuwa mitume wa upendo. Kwa mfano wenu, mtawafanya wale wanangu wasiomjua Mwanangu
na
upendo wake watake kumjua. Wanangu, mitume wa upendo wangu, mwabuduni Mwanangu pamoja nami,
na
mpendeni juu ya vyote. Jaribuni sikuzote kuishi katika ukweli wake. Ninawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2019
“
W
anangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali. Sala iwe manukato kwa roho zenu kwani tunda la sala ni furaha, kutoa, kumshuhudia Mungu kwa wengine kwa njia ya maisha yenu. Wanangu, mkimtegemea Mungu kabisa, Yeye atashughulika yote, atawabariki
na
sadaka zenu zitapata maana. Mimi nipo pamoja nanyi
na
ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2019 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, Mwanangu mpenzi alimwomba sikuzote
na
kumtukuza Baba wa Mbinguni. Sikuzote alikuwa amemwambia yote
na
kujiachia katika mapenzi yake. Hivyo mnapaswa kufanya hata ninyi, wanangu, maana Baba wa Mbinguni anawasikiliza sikuzote wanawe. Moyo wa umoja katika moyo mmoja: upendo, mwanga
na
uhai. Baba wa Mbinguni amejitolea kwa njia ya sura ya kibinadamu,
na
sura ile ndiyo sura ya Mwanangu. Ninyi, mitume wa upendo wangu, ninyi mnapaswa sikuzote kupokea sura ya Mwanangu katika mioyo yenu
na
katika fikira zenu. Ninyi mnapaswa sikuzote kuufikiria upendo wake
na
sadaka yake. Mnapaswa kusali ili kusudi mwone uwepo wake sikuzote. Maana, enyi mitume wa upendo wangu, hii ni jinsi ya kuwasaidia wale wote wasiomjua Mwanangu, wale ambao hawajajua upendo wake. Wanangu, someni kitabu cha Injili: ni sikuzote kitu kipya, ni kinachowaunganisha
na
Mwanangu, aliyezaliwa kwa kuwaletea maneno ya uzima wanangu wote
na
kwa kujitoa sadaka kwa ajili ya wote. Mitume wa upendo wangu, mkisukumwa
na
upendo kumwelekea Mwanangu, leteni upendo
na
amani kwa ndugu zenu wote. Msimhukumu mtu, pendeni kila mtu kwa njia ya upendo kwa kumwelekea Mwanangu. Hivyo mtashughulika hata
na
roho zenu, nayo ni yenye thamani kuliko kitu chochote mlicho nacho. Ninawashukuru.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
Next>>