Our Lady of Medjugorje Messages containing 'ufufuko'
Total found:
2
Ujumbe, 2 Aprili 2015 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nimewachagua ninyi, mitume wangu, kwa maana kila mmoja wenu huchukua ndani yake jambo njema. Ninyi mnaweza kunisaidia ili ule upendo ambao kwao Mwanangu amekufa, na kufufuka baadaye, ushinde tena. Kwa hiyo nawaalika, mitume wangu, kujaribu kuona katika kila kiumbe cha Mungu, katika wanangu wote, kitu chema na kujitahidi kuwaelewa. Wanangu, ninyi nyote ni kaka na dada kwa njia ya huyo Roho Mtakatifu. Ninyi mliojaa upendo kwa ajili ya Mwanangu, mnaweza kuwaeleza wote ambao hawajui cho chote kuhusu upendo huo, yote mnayoyafahamu. Ninyi mmejua upendo wa Mwanangu, mnaelewa
ufufuko
wake, na mnamgeuzia macho kwa furaha. Haja yangu ya kimama ni kwamba wanangu wote waungane katika upendo wa Yesu. Kwa hiyo nawaalika, mitume wangu, kuishi kwa furaha Ekaristi maana, katika Ekaristi, mwanangu anajitoa kwa ajili yenu tena na tena, na kwa mfano wake, anawaonyesha namna ya kutoa upendo na sadaka kwa jirani. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2018
“
W
anangu wapendwa, leo pia ninawaalika kuishi pamoja na Yesu maisha yenu mapya. Bwana Mfufuka awape nguvu ili muwe daima mashujaa katika majaribu ya maisha, na waaminifu na mdumu katika kusali, maana Yesu aliwaokoeni kwa majeraha Yake na kwa njia ya
Ufufuko
Wake aliwapa maisha mapya. Salini, wanangu na msipoteze matumaini. Katika mioyo yenu na ziwe furaha na amani, muwe mashahidi ya furaha ya kuwa wangu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose