Our Lady of Medjugorje Messages containing 'uongofu'
Total found:
7
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao Mungu anawajalia kwa njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa
uongofu
binafsi na kwenye sala katika familia zenu. Maandiko matakatifu yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni nyote kusali. Fungueni kwa kina mlango wa mioyo yenu, enyi wanangu, kwa sala, sala ya moyo na hivyo Yeye Aliye Juu ataweza kufanya kazi katika uhuru wenu na kuanzisha
uongofu
wenu. Hivyo imani yenu itakuwa imara kiasi cha kuweza kusema kwa moyo wenu wote: "Mungu wangu na yote yangu". Halafu mtaweza kuelewa, wanangu, ya kuwa duniani hapa yote hupita. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Mei 2017
“
W
anangu wapendwa! Yeye Aliye juu ameniruhusu kuwaalikeni tena kwa
uongofu
. Wanangu, fungueni mioyo yenu kwa neema ambayo wote mnaalikwa. Muwe mashahidi wa amani na wa upendo katika ulimwengu huu wa wasiwasi. Maisha yenu hapa duniani ni ya mpito. Salini ili kwa njia ya sala muweze kutamani mbingu na mambo ya mbinguni na mioyo yenu itaona yote kwa njia tofauti. Ninyi si peke yenu, Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombeeni kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2022
“
W
anangu wapendwa! Niko pamoja nanyi kuwaongoza katika njia ya
uongofu
kwa sababu, wanangu, kwa maisha yenu mnaweza kuleta nafsi nyingi karibu na Mwanangu. Iweni mashahidi wenye furaha wa Neno la Mungu na wa upendo, mkiwa na matumaini ndani ya mioyo yenu yashindayo uovu wote. Mwasamehe wanaowadhuru na tembeeni katika njia ya utakatifu. Ninawaongoza kwa Mwanangu ili Yeye awe njia, ukweli na uzima kwenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2022
“
W
anangu wapendwa! Aliye juu amenituma kwenu ili niwafundishe jinsi ya kuomba. Sala hufungua mioyo na kutoa tumaini; imani huzaliwa na kuimarishwa. Wanangu, nawaiteni kwa upendo: mrudieni Mungu kwa maana Mungu ni upendo wenu na tumaini lenu. Msipoamua kwa ajili ya Mungu hamna mustakabali na kwa hiyo niko pamoja nanyi kuwaongoza ili muamue
uongofu
na uzima na sio kifo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Julai 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ambao Aliye Juu amenituma niwapende ninyi na kuwaongoza katika njia ya
uongofu
, toeni sala zenu na sadaka zenu kwa ajili ya wale wote walio mbali na wasiojua upendo wa Mungu. Ninyi, wanangu, muwe mashahidi wa upendo na amani kwa mioyo yote isiyotulia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2023
“
W
anangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya
uongofu
wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose