Our Lady of Medjugorje Messages containing 'upepo'
Total found:
5
Ujumbe, 25 Oktoba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni mjifungulie kwa sali. Sala itasababisha miujiza ndani yenu na kwa njia yenu. Kwa hiyo, enyi wanangu, kwa moyo mkunjufu mtafuteni Yeye Aliye Juu ili awapeni nguvu ya kuwa wana wa Mungu, na yule Shetani asiwatikiseni kama matawi yatikiswavyo na
upepo
. Kateni shauri tena, wanangu, kwa Mungu na tafuteni tu mapenzi yake, hapo mtapata furaha na amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Januari 2015
“
W
anangu wapendwa! Hata leo ninawaalika: ishini katika sala mwito wenu. Leo, kama bado haijatokea awali, Shetani atamani kumfunga pumzi binadamu na roho yake kwa njia ya
upepo
wake unaoambukiza chukio na hofu. Katika mioyo mingi hakuna furaha kwa sababu hakuna Mungu wala sala. Uadui na vita zinaongezeka siku hata siku. Ninawaalika, wanangu, anzisheni upya kwa ari mwelekeo wa kutafuta utakatifu na upendo kwa maana nimekuja katikati yenu kwa ajili hiyo. Tuwe upendo na msamaha kwa wale wote wanaofahamu na kutaka kupenda kwa mapendo ya kibinadamu tu wala siyo kwa ule upendo mkubwa sana wa kimungu ambao Mungu anatualikia. Wanangu, matumaini ya kesho iliyo bora zaidi yawe daima mioyoni mwenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2016
“
W
anangu wapendwa! Leo nataka kushirikiana pamoja nanyi furaha ya mbinguni. Ninyi wanangu fungueni mlango wa moyo ili katika moyo wenu matumaini, amani na mapendo ambazo Mungu peke yake anaweza kutoa ziweze kukua. Wanangu, mnapenda mno dunia na mambo ya dunia, kwa hiyo Shetani huwatikisa kama
upepo
ufanyavyo na mawimbi ya bahari. Kwa hiyo mnyororo wa maisha yenu uwe sala ya moyo na kumwabudu Mwanangu Yesu. Kwake mtolee maisha yenu yajayo ili muwe ndani Yake furaha na mfano kwa watu wengine kwa njia ya matendo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Februari 2017
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalika kuishi kwa kina imani yenu na kumwomba Aliye juu ili aiimarishe, hivyo
upepo
na dhoruba yasije yakaivunja. Mizizi ya imani yenu iwe sala na tumaini katika uzima wa milele. Tokea sasa, wanangu, jijengeni wenyewe, katika wakati huu wa neema ambapo Mungu anawapeni neema ili kwa njia ya kujinyima na mwito wa kuongoka muwe watu wenye imani na tumaini safi na ya kuvumilia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
Ujumbe, 25 Aprili 2019
“
W
anangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema, wakati wa rehema kwa kila mmoja wenu. Wanangu, msiruhusu
upepo
wa chukio na hofu utawale ndani yenu na karibu nanyi. Ninyi, wanangu, mmealikwa kuwa upendo na sala. Ibilisi ataka hofu na fujo lakini ninyi, wanangu, muwe furaha ya Yesu Mfufuka ambaye amekufa na kufufuka kwa ajili ya kila mmoja wenu. Yeye ameshinda kifo kwa kuwapeni uzima, uzima wa milele. Kwa hiyo, wanangu, mshuhudieni na muwe wenye fahari kwa kufufuliwa katika Yeye. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose