Ujumbe, 25 Januari 2023
“Wanangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana shetani anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili Mungu awape amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu wa kisasa hataki Mungu. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu, ni tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira yenu na muwe watu wa amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”