| Search this website | ||||
Ujumbe, 2 Septemba 2013 - MirjanaOther languages: English, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Norsk, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt
“Wanangu wapendwa, nawapendeni, ninyi nyote, watoto wangu nyote, muwe wote moyoni mwangu, ninyi nyote mmepata upendo wangu wa kimama na ninatamani kuwaongoza nyote ili mjue furaha ya Mungu. Kwa hiyo nawaalikeni: nahitaji mitume wanyenyekevu ambao, kwa moyo mkunjufu, wanapokea Neno la Mungu na ambao wako tayari kuwasaidia watu wengine ili, kwa njia ya Neno la Mungu, waelewe maana ya maisha yao. Ili muweze kufanya hayo, wanangu, yawapasa, kwa njia ya kusali na kufunga, kusikiliza kwa moyo mkunjufu na kujifunza kujidhili au kujinyenyekesha. Yawapasa kujifunza kukataa yote yanayowatenganisha na Neno la Mungu na kutamani tu yanayowakaribisha. Msiogope, mimi nipo hapa. Ninyi si peke yenu. Namwomba Roho Mtakatifu ili awafanye wapya, ili awaimarishe. Namwomba Roho Mtakatifu, ili mkisaidia wengine, muweze kujiponya nyinyi wenyewe. Naomba ili, kwa njia yake, muwe wana wa Mungu na mitume wangu. ” Kisha kwa mahangaiko makubwa Bikira Maria alisema: “Kwa ajili ya Yesu, kwa ajili ya mwanangu, pendeni wale ambao Yeye aliwaita mkitamani baraka ya mikono ile ambayo Yeye tu ameyaweka wakfu. Msiyaruhusu maovu yatawale. Nawaalikeni tena: ni kwa njia ya wachungaji wangu tu moyo wangu utashinda. Msiyaruhusu maovu yawatenganisheni na wachungaji wenu. Nawashukuru. ” To compare Medjugorje messages with another language versions choose | | |||
|
Our Lady of Medjugorje Messages ![]() Find messages Enter words or phrase Random Messages “Today I invite all of you who have heard my message of peace to realize it with seriousness and with love in your life. There are many who think that they are doing a lot by talking about the messages, but do not live them.” ( From message, 25 Mei 1991 ) | Medjugorje Live Current time in Medjugorje (CET): Deep concern & disturbing information: Latest news & articles 25 Septemba 2024 Latest videos 11 Juni 2018 10 Mei 2018 13 Aprili 2018 31 Machi 2018 16 Machi 2018 Most read articles Most watched videos Most watched Medjugorje Photos Gallery albums ![]() Favorite content related to Medjugorje" | |||
| Our Lady of Medjugorje Messages Medjugorje News & Articles Medjugorje Videos Medjugorje Web Sites Links Picture & Photo Galleries The Polls | Copyright © 2005-2026 Medjugorje WebSite medjugorje.ws medjugorie.ws medugorje.ws ourlady.eu and content contributors | |||
![[EN]](/data/default/css/img/en-only.gif)
![[O]](/data/olm/images/__mt/nw.gif)
