| Search this website | ||||
Ujumbe, 2 Januari 2017 - Tokeo la MirjanaOther languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Mwanangu alikuwa chemchemi ya upendo na mwanga alipoongea na watu wa mataifa yote. Mitume wangu, fuateni mwanga wake, si rahisi, yawapasa kuwa wadogo, yawapasa kuwa wadogo kuliko wengine wote na kwa msaada wa imani kujazwa na upendo wake. Hakuna mtu duniani, pasipo imani, awezaye kuwa na uzoefu wa mwujiza. Mimi nipo pamoja nanyi, ninajionyesha kwa matokeo hayo, kwa maneno hayo, nataka kuwashuhudia upendo wangu na utunzaji wangu wa kimama. Wanangu, msipoteze wakati mkiweka maswali ambayo hamtapata kamwe majibu, maisha yenu duniani yatakapomalizika Baba wa Mbinguni atawajibu. Mjue daima ya kuwa Mungu hujua yote, Mungu huona, Mungu hupenda. Mwanangu mpenzi sana huangaza maisha na kupasua giza. Upendo wa kimama unaonileta kwenu hauelezeki, umefichwa lakini ni halisi, ninawaonyesheni hisia zangu, upendo, hisani na ukarimu wangu wa kimama. Kutoka kwenu, mitume wangu, ninatafuta sala zenu: mawaridi yaliyo matendo ya upendo, hizo ndizo kwa moyo wangu wa kimama sala za kunipendeza sana, haya ninayaletea Mwanangu aliyezaliwa kwa ajili yenu. Yeye anawatazama ninyi na kuwasikia. Sisi tupo kila siku karibu nanyi kwa upendo wenu ambao huita, huunga, huongoa, hutia moyo na kujaza. Kwa hiyo mitume wangu pendaneni daima, lakini hasa mpende Mwanangu, hii ni njia ya pekee ya wokovu kuelekea uzima wa milele, hiyo ni sala ya kunipendeza ambayo kama harufu nzuri ajabu ya mawaridi, hujaa moyo wangu. Ombeni daima, waombeeni wachungaji wenu ili wapate nguvu ya kuwa mwanga wa Mwanangu. Nawashukuru. ” To compare Medjugorje messages with another language versions choose | | |||
|
This page Our Lady of Medjugorje Messages ![]() Find messages Enter words or phrase Random Messages “Little children, I invite you again to decide for prayer because through prayer, you will be able to live the conversion. Each one of you shall become in the simplicity, similar to a child which is open to the love of the Father.” ( From message, 25 Julai 1996 ) |
Medjugorje Live Current time in Medjugorje (CET): Deep concern & disturbing information: Latest news & articles 25 Septemba 2024 Latest videos 11 Juni 2018 10 Mei 2018 13 Aprili 2018 31 Machi 2018 16 Machi 2018 Most read articles Most watched videos Most watched Medjugorje Photos Gallery albums ![]() Favorite content related to Medjugorje" | |||
| Our Lady of Medjugorje Messages Medjugorje Web Sites Links Medjugorje News & Articles Medjugorje Videos Picture & Photo Galleries The Polls | Copyright © 2005-2026
| |||
![[EN]](/data/default/css/img/en-only.gif)
![[O]](/data/olm/images/__mt/nw.gif)
