Our Lady of Medjugorje Messages containing 'machukio'

Total found: 5
Wanangu wapendwa, Namshukuru Mungu kwa kila mmoja wenu. Hasa, wanangu, asanteni kwa kuitikia wito wangu. Mimi ninawatayarisha kwa nyakati mpya ili muwe imara katika imani na kusali daima, ili Roho Mtakatifu atende kwa njia yenu na afanye upya uso wa nchi. Ninasali pamoja nanyi kwa amani, karama ya thamani kuliko zote, hata ingawa shetani hutaka vita na machukio. Ninyi, wanangu, muwe mikono yangu inayonyoshwa na tembeeni katika kujivunia pamoja na Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu wakati wa sala. Bila Mungu hamwezi kuwa na amani. Kwa hiyo, wanangu, salini kwa ajili ya amani katika mioyo yenu na katika familia zenu ili Yesu aweze kuzaliwa ndani yenu na kuwapeni upendo wake na baraka yake. Ulimwengu uko katika vita kwa sababu mioyo imejaa machukio na wivu. Wanangu, wasiwasi unaonekana katika macho yenu kwa sababu hamkuruhusu Yesu kuzaliwa katika maisha yenu. Mtafuteni, ombeni na Yeye atajitoa kwenu katika yule Mtoto aliye furaha na amani. Mimi niko pamoja nanyi na ninasali pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Katika wakati huo ninawaalika kusali, kufunga na kujikana ili muweze kuwa wenye nguvu zaidi katika imani. Huu ni wakati wa mwamko na wa kuzaliwa upya. Kama vitu vya asili vinavyojitoa nanyi wanangu, fikirini juu ya mambo mliyopokea. Muwe waletaji wa amani na wa upendo wenye furaha ili kuishi vizuri duniani. Tamanini Mbingu kwa sababu Mbinguni hakuna wala huzuni wala machukio. Kwa hiyo, wanangu, amueni tena kuongoka, na utakatifu utawale katika maisha yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Kwa furaha ninawaalika ninyi nyote, wanangu, mlioitikia wito wangu, kuwa furaha na amani. Kwa maisha yenu shuhudieni Mbingu ninayowaletea. Ni saa, wanangu, ya kuwa wonyesho wa upendo wangu kwa wote wale ambao hawapendi na mioyo yao imeshindwa na machukio. Msisahau: mimi ni pamoja nanyi na ninawaombea ninyi nyote karibu na mwanangu Yesu ili awapeni amani yake. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ninafurahi pamoja nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa makusudi yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika mpango wangu wa wokovu wa wanadamu. Rudeni kwa Mungu na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu, Mimi ni pamoja nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
   




To compare Medjugorje messages with another language versions choose

For God to live in your hearts, you must love.

`