| | Medjugorje Website Updates
Languages: English, Afrikaans, العربية, Български, Беларуская, Català, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Malti, Nederlands, Norsk, Polski, Português, Română, Русский, Shqip, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Svenska, Tagalog, Tiếng Việt, Українська, زبان_فارسی
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu himizo kwa wongofu wenu binafsi. Wanangu, ombeni katika upweke Roho Mtakatifu ili iwaimarishe katika imani na katika kumsadiki Mungu ili kuweza kuwa mashahidi wa upendo ambao Mungu anawapa kupitia uwepo wangu. Wanangu, msiruhusu majaribu yafanye mioyo yenu kuwa migumu na sala kuwa kama jangwa. Muwe mwangi wa upendo wa Mungu na mshuhudieni Yesu Aliyefufuka kwa njia ya maisha yenu. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawapenda nyote kwa upendo wangu wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, katika miaka hii yote mimi nipo pamoja nanyi ili kuwaongoza kwenye njia ya wokovu. Rudieni kwa Mwanangu, rudieni katika sala na mfungo. Wanangu, mwachieni Mungu aongee na mioyo yenu kwa sababu shetani anatawala na anatamani kuangamiza maisha yenu na dunia mnamotembelea. Muwe na ujasiri na amueni kuwa watakatifu. Mtaona wongofu katika mioyo yenu na katika familia zenu, sala itasikilizwa, Mungu atayapokea maombi yenu na kuwapa amani. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, upendo wenu safi na wa kweli unavuta Moyo wangu wa kimama. Imani yenu na usadiki wenu katika Baba wa mbinguni ni mawaridi yenye harufu nzuri mnayonitolea: shada la mawaridi mazuri sana, lililotengenezwa kwa sala zenu, kwa matendo ya rehema na ya upendo. Mitume wa upendo wangu, ninyi mnaojaribu kumfuata Mwanangu pasipo unafiki na kwa moyo safi, ninyi ambao pasipo unafiki mnampenda, muwe ninyi wenyewe kusaidia: muwe mfano kwa wale ambao hawajajua upendo wa Mwanangu. Lakini, wanangu, siyo kwa maneno tu, bali hata kwa matendo na hisia safi, ambayo kwa njia yake mnamtukuza Baba wa mbinguni. Mitume wa upendo wangu, ni wakati wa kukesha na ninawaombeni upendo; na msihukumu mtu yeyote, kwa maana Baba wa mbinguni atahukumu wote. Ninawaombeni mpende, na mueneze ukweli, kwa maana ukweli ni wa kale: Ukweli siyo mpya, Ukweli ni wa milele, Ukweli ndiyo ukweli! Ukweli unatolea ushuhuda wa umilele wa Mungu. Bebeni mwanga wa Mwanangu na mpasue giza ambalo linataka kuwakandamiza zaidi na zaidi. Msiwe na hofu: kwa ajili ya neema na upendo wa Mwanangu, mimi nipo pamoja nanyi! Ninawashukuru. ””
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Katika kipindi hiki cha neema nataka kuona nyuso zenu zigeuke katika sala. Ninyi mmejaa mahangaiko ya kidunia kiasi kwamba hamuoni hata ujio wa majira ya kuchipua kwa mimea. Wanangu, mnaalikwa kwa toba na kwa sala. Kama viumbe vya asili vinapigana katika kimya kwa maisha mapya, hivyo hata ninyi mnaalikwa kujifungua katika sala kwa Mungu ambaye kwake mtapata amani na joto la jua la kipindi cha kuchanua kwa mimea katika mioyo yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, nilichaguliwa kuwa mama wa Mungu na mama yenu, kwa maamuzi na upendo wa Bwana, lakini pia kwa mapenzi yangu, kwa upendo wangu usio na kifani kwake Baba wa mbinguni na kwa imani yangu yote Kwake. Mwili wangu ulikuwa kikombe cha Mungu Mtu. Nilikuwa mtumishi wa ukweli, wa upendo na wokovu kama vile nilivyo sasa katikati yenu, ili kuwaalika, wanangu, mitume wa upendo wangu, kuwa waletaji ukweli, ili kuwaalika, kwa njia ya utashi na upendo yenu kumwelekea Mwanangu, ili kueneza maneno Yake, maneno ya wokovu na kuyaonyesha, kwa vitendo vyenu, kwa wale wote ambao hawajamjua mwanangu na upendo Wake. Nguvu mtaipata katika Ekaristi: Mwanangu awalisheni kwa mwili Wake na kuwaimarisha kwa damu Yake. Wanangu, wekeni mikono yenu pamoja kwa sala na tazameni kuelekea msalaba kwa ukimya. Kwa jinsi hii mtapata imani ili muweze kuieneza, mtapata ukweli ili muweze kuupambanua, mtapata upendo ili muweze kuelewa namna ya kupenda kwa uhakika. Wanangu, mitume wa upendo wangu, wekeni mikono yenu pamoja kwa sala na tazameni kuelekea msalaba: katika msalaba tu kuna wokovu. Ninawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali tena zaidi ili msikie katika mioyo yenu utakatifu wa msamaha. Katika familia lazima kuwepo utakatifu kwa sababu enyi wanangu, ulimwengu hauna wakati ujao bila upendo na utakatifu, kwa sababu katika utakatifu na katika furaha ninyi mjitolee kwa Mungu Mwumbaji anayewapendeni kwa upendo mkubwa sana. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, najua kuwepo katika maisha yenu na mioyo yenu. Nahisi upendo wenu, nasikia sala zenu na kuzipeleka kwa Mwanangu. Lakini, wanangu, mimi nataka kwa njia ya upendo wa kimama, kuwepo katika maisha ya wanangu wote. Nataka kukusanya karibu yangu wanangu wangu wote, chini ya joho langu la kimama. Kwa hiyo ninawaalika ninyi na kuwaiteni mitume wa upendo wangu, il mnisaidie. Wanangu, Mwanangu aliyatamka maneno haya: "Baba yetu”, Baba yetu uliye popote na katika mioyo yetu, kwa sababu ataka kuwafundisha kusali kwa maneno na kwa hisia zenu. Ataka muwe bora zaidi kila siku, muishi upendo wenye rehema ulio sala na sadaka isiyo na mipaka kwa ajili ya wengine. Wanangu mpeni Mwanangu upendo kwa jirani; mpeni jirani wenu maneno ya faraja, ya huruma na matendo ya haki. Yote mliyoyatoa kwa wengine, enyi mitume wa upendo wangu, Mwanangu anayapokea kama zawadi. Nami ni pamoja nanyi kwa sababu Mwanangu ataka kwamba upendo wangu, ulio kama mwali wa nuru, uzihuishe nafsi zenu, uwasaidie katika kutafuta amani na uheri wa milele. Kwa hiyo, wanangu, pendaneni, na muunganishwe kwa njia ya Mwanangu, ili muwe wana wa Mungu ambao wote pamoja kwa moyo uliojaa, wazi na safi mkisema kwa pamoja “Baba yetu” pasipo kuogopa! Ninawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Nawaletea ninyi Mwanangu Yesu ili awabariki na kuwafunulia Upendo wake utokao mbinguni. Moyo wenu unatamani amani inayopungua zaidi na zaidi duniani. Kwa sababu hiyo watu wako mbali na Mungu, nafsi zinaumwa na zinaelekea kifo cha kiroho. Mimi nipo pamoja nanyi, wanangu, niwaongoze kwenye njia hii ya wokovu ambayo Mungu anawaiteni. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, ninapowatazama ninyi mnaopenda Mwanangu, furaha inajaza Moyo wangu. Ninawabariki kwa baraka ya kimama. Pamoja na baraka ya kimama ninawabariki hata wachungaji wenu: ninyi mnaotangaza maneno ya Mwanangu, mnaobariki kwa mikono yake na mnaompenda hata kuwa tayari kufanya kwa furaha kila sadaka kwa ajili yake. Ninyi mfuateni Yeye, aliyekuwa Mchungaji wa kwanza, Mmisionari wa kwanza. Wanangu, mitume wa upendo wangu, kuishi na kufanya kazi kwa ajili ya wengine, kwa wale wote mnaopenda kwa njia ya Mwanangu, ni furaha na faraja ya maisha ya kidunia. Ikiwa kwa njia ya sala, upendo na sadaka Ufalme wa Mungu ni katika mioyo yenu, hapo kwa ninyi maisha ni yenye furaha na matulivu. Katikati ya wale wanaompenda Mwanangu na wanaopendana kwa ajili yake, maneno si ya lazima. Kutazamana kwatosha ili kusikia maneno yasiyonenwa na hisia zisizoonyeshwa. Pale panapotawala upendo, wakati hauna maana tena. Sisi ni pamoja nanyi! Mwanangu anawajua na kuwapenda. Upendo ni kilichowaongoza kwangu na, kwa njia ya upendo huu, mimi nitakuja kwenu na nitawaambieni kazi za wokovu. Ninataka ya kuwa wana wangu wote wawe na imani na wahisi upendo wangu wa kimama unaowaongoza kwa Yesu. Kwa hiyo ninyi, wanangu, ko kote mwendako angazeni kwa upendo na kwa imani, kama mitume wa upendo. Ninawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, wakati huu uwe kwenu wakati wa sala. Bila Mungu hamwezi kuwa na amani. Kwa hiyo, wanangu, salini kwa ajili ya amani katika mioyo yenu na katika familia zenu ili Yesu aweze kuzaliwa ndani yenu na kuwapeni upendo wake na baraka yake. Ulimwengu uko katika vita kwa sababu mioyo imejaa machukio na wivu. Wanangu, wasiwasi unaonekana katika macho yenu kwa sababu hamkuruhusu Yesu kuzaliwa katika maisha yenu. Mtafuteni, ombeni na Yeye atajitoa kwenu katika yule Mtoto aliye furaha na amani. Mimi niko pamoja nanyi na ninasali pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Mwanangu mpenzi alimwomba sikuzote na kumtukuza Baba wa Mbinguni. Sikuzote alikuwa amemwambia yote na kujiachia katika mapenzi yake. Hivyo mnapaswa kufanya hata ninyi, wanangu, maana Baba wa Mbinguni anawasikiliza sikuzote wanawe. Moyo wa umoja katika moyo mmoja: upendo, mwanga na uhai. Baba wa Mbinguni amejitolea kwa njia ya sura ya kibinadamu, na sura ile ndiyo sura ya Mwanangu. Ninyi, mitume wa upendo wangu, ninyi mnapaswa sikuzote kupokea sura ya Mwanangu katika mioyo yenu na katika fikira zenu. Ninyi mnapaswa sikuzote kuufikiria upendo wake na sadaka yake. Mnapaswa kusali ili kusudi mwone uwepo wake sikuzote. Maana, enyi mitume wa upendo wangu, hii ni jinsi ya kuwasaidia wale wote wasiomjua Mwanangu, wale ambao hawajajua upendo wake. Wanangu, someni kitabu cha Injili: ni sikuzote kitu kipya, ni kinachowaunganisha na Mwanangu, aliyezaliwa kwa kuwaletea maneno ya uzima wanangu wote na kwa kujitoa sadaka kwa ajili ya wote. Mitume wa upendo wangu, mkisukumwa na upendo kumwelekea Mwanangu, leteni upendo na amani kwa ndugu zenu wote. Msimhukumu mtu, pendeni kila mtu kwa njia ya upendo kwa kumwelekea Mwanangu. Hivyo mtashughulika hata na roho zenu, nayo ni yenye thamani kuliko kitu chochote mlicho nacho. Ninawashukuru. ”
10 Novemba 2006 , Last update 27 Oktoba 2019 / Section: Medjugorje - Category: Section Documents
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali. Sala iwe manukato kwa roho zenu kwani tunda la sala ni furaha, kutoa, kumshuhudia Mungu kwa wengine kwa njia ya maisha yenu. Wanangu, mkimtegemea Mungu kabisa, Yeye atashughulika yote, atawabariki na sadaka zenu zitapata maana. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, mapenzi na upendo wa Baba wa mbinguni hufanya mimi niwe katikati yenu, ili kusaidia kwa upendo wa kimama ukuaji wa imani katika mioyo yenu, ili kwamba muweze hakika kuelewa lengo la maisha ya kidunia na ukuu wa yale ya kimbingu. Wanangu, maisha ya kidunia ndiyo njia kuelekea umilele, kuelekea ukweli na uzima: kuelekea kwa Mwanangu. Kwa njia hii nataka kuwaongoza. Ninyi, wanangu, ninyi wenye sikuzote kiu ya upendo mkubwa zaidi, ukweli na imani, mjue ya kuwa moja tu ni chemchemi mnakoweza kunywa: imani katika Baba wa mbinguni, imani katika upendo wake. Mtegemee kabisa mapenzi yake wala msiogope: kila lililo bora kwa ajili yenu, kila linalowachukua kwenye uzima wa milele, mtapewa! Mtaelewa ya kuwa lengo la maisha si sikuzote kutaka na kutwaa, lakini kupenda na kutoa; mtakuwa na amani ya kweli na upendo wa kweli, mtakuwa mitume wa upendo. Kwa mfano wenu, mtawafanya wale wanangu wasiomjua Mwanangu na upendo wake watake kumjua. Wanangu, mitume wa upendo wangu, mwabuduni Mwanangu pamoja nami, na mpendeni juu ya vyote. Jaribuni sikuzote kuishi katika ukweli wake. Ninawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Leo ninawaalika kusali kwa ajili ya makusudi yangu ili niweze kuwasaidia. Wanangu, salini Rosari mkitafakari mafumbo ya Rosari maana hata ninyi katika maisha yenu mnapitia furaha na maumivu. Kwa njia hii mtageuza mafumbo katika maisha yenu maana maisha ni fumbo hadi mtakapoyaweka katika mikono ya Mungu. Hivyo mtakuwa na mang'amuzi ya imani kama Petro aliyemkuta Yesu na Roho Mtakatifu aliyoijaza roho yake. Hata ninyi, wanangu, mnaalikwa kushuhudia mkiishi upendo ambao kwao siku kwa siku Mungu anawajaza kwa njia ya uwepo wangu. Kwa hiyo, wanangu, muwe wazi na salini kwa moyo katika imani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
| | |