Our Lady of Medjugorje Messages containing 'kiumbe'

Total found: 3
Wanangu wapendwa, nimewachagua ninyi, mitume wangu, kwa maana kila mmoja wenu huchukua ndani yake jambo njema. Ninyi mnaweza kunisaidia ili ule upendo ambao kwao Mwanangu amekufa, na kufufuka baadaye, ushinde tena. Kwa hiyo nawaalika, mitume wangu, kujaribu kuona katika kila kiumbe cha Mungu, katika wanangu wote, kitu chema na kujitahidi kuwaelewa. Wanangu, ninyi nyote ni kaka na dada kwa njia ya huyo Roho Mtakatifu. Ninyi mliojaa upendo kwa ajili ya Mwanangu, mnaweza kuwaeleza wote ambao hawajui cho chote kuhusu upendo huo, yote mnayoyafahamu. Ninyi mmejua upendo wa Mwanangu, mnaelewa ufufuko wake, na mnamgeuzia macho kwa furaha. Haja yangu ya kimama ni kwamba wanangu wote waungane katika upendo wa Yesu. Kwa hiyo nawaalika, mitume wangu, kuishi kwa furaha Ekaristi maana, katika Ekaristi, mwanangu anajitoa kwa ajili yenu tena na tena, na kwa mfano wake, anawaonyesha namna ya kutoa upendo na sadaka kwa jirani. Nawashukuru.
Wanangu wapendwa! Rudieni kusali maana wanaosali hawaogopi wakati ujao. Wale wanaosali wako wazi kwa uzima na wanaheshimu maisha ya wengine. Yeyote anayesali, wanangu, anahisi uhuru wa wana wa Mungu na kwa moyo wa furaha hutumikia kwa manufaa ya ndugu yake. Kwa sababu Mungu ni upendo na uhuru. Kwa hiyo, wanangu, wanapotaka kuwafunga kwa minyororo na kuwatumia hilo halitoki kwa Mungu maana Mungu ni upendo na humpa kila kiumbe amani yake. Kwa hiyo amenituma niwasaidie ninyi kukua katika njia ya utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ninawaalika ninyi mwende katika mazingira ya asili na kusali ili kwamba Aliye Juu Sana aseme na moyo wenu na kwamba muweze kuhisi uwezo wa Roho Mtakatifu kushuhudia upendo ambao Mungu anao kwa kila kiumbe. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
   




To compare Medjugorje messages with another language versions choose

For God to live in your hearts, you must love.

`