Our Lady of Medjugorje Messages containing 'imani'

Total found: 66
Wanangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati huu wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu mimi niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu awapeni amani yake. Wanangu, bila amani hamna wala wakati ujao, wala baraka, kwa hiyo rudieni kusali kwa sababu tunda la sala ni furaha na imani, na bila hiyo hamwezi kuishi. Baraka ya leo tunayowapa, ileteni kwa jamaa zenu na tajirisheni wote wale mnaokuta ili wahisi neema ambayo mnapokea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Mungu ananiruhusu niwe pamoja nanyi na kuwaongoza kwenye njia ya amani ili kupitia amani ya kibinafsi, muweze kujenga amani duniani. Nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa Mwanangu Yesu ili awape imani thabiti na tumaini ya maisha bora ya baadaye ninayotaka kujenga pamoja nanyi. Ninyi, jipeni moyo na msiogope maana Mungu yu pamoja nanyi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Aliye juu aliniruhusu niwe pamoja nanyi; kuwa furaha kwenu na njia katika matumaini kwa sababu ubinadamu umeamua kifo. Kwa hiyo amenituma niwaelekeze kwamba bila Mungu hamna wakati ujao. Wanangu, muwe vyombo vya upendo kwa wale wote ambao hawajamjua Mungu wa upendo. Kwa furaha toeni ushuhuda wa imani yenu na msipoteze matumaini katika mabadiliko ya moyo wa mwanadamu. Niko pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka yangu ya mama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Aliye juu amenituma kwenu ili niwafundishe jinsi ya kuomba. Sala hufungua mioyo na kutoa tumaini; imani huzaliwa na kuimarishwa. Wanangu, nawaiteni kwa upendo: mrudieni Mungu kwa maana Mungu ni upendo wenu na tumaini lenu. Msipoamua kwa ajili ya Mungu hamna mustakabali na kwa hiyo niko pamoja nanyi kuwaongoza ili muamue uongofu na uzima na sio kifo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
   




To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous  1 2 3 4

For God to live in your hearts, you must love.

`