Search this website | ||||
![]() | ![]() | ![]() | ![]() | ![]() |
![]() | Ujumbe, 2 Desemba 2019 - Tokeo la MirjanaOther languages: English, العربية, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, ninapowatazama ninyi mnaopenda Mwanangu, furaha inajaza Moyo wangu. Ninawabariki kwa baraka ya kimama. Pamoja na baraka ya kimama ninawabariki hata wachungaji wenu: ninyi mnaotangaza maneno ya Mwanangu, mnaobariki kwa mikono yake na mnaompenda hata kuwa tayari kufanya kwa furaha kila sadaka kwa ajili yake. Ninyi mfuateni Yeye, aliyekuwa Mchungaji wa kwanza, Mmisionari wa kwanza. Wanangu, mitume wa upendo wangu, kuishi na kufanya kazi kwa ajili ya wengine, kwa wale wote mnaopenda kwa njia ya Mwanangu, ni furaha na faraja ya maisha ya kidunia. Ikiwa kwa njia ya sala, upendo na sadaka Ufalme wa Mungu ni katika mioyo yenu, hapo kwa ninyi maisha ni yenye furaha na matulivu. Katikati ya wale wanaompenda Mwanangu na wanaopendana kwa ajili yake, maneno si ya lazima. Kutazamana kwatosha ili kusikia maneno yasiyonenwa na hisia zisizoonyeshwa. Pale panapotawala upendo, wakati hauna maana tena. Sisi ni pamoja nanyi! Mwanangu anawajua na kuwapenda. Upendo ni kilichowaongoza kwangu na, kwa njia ya upendo huu, mimi nitakuja kwenu na nitawaambieni kazi za wokovu. Ninataka ya kuwa wana wangu wote wawe na imani na wahisi upendo wangu wa kimama unaowaongoza kwa Yesu. Kwa hiyo ninyi, wanangu, ko kote mwendako angazeni kwa upendo na kwa imani, kama mitume wa upendo. Ninawashukuru. ” To compare Medjugorje messages with another language versions choose | | ![]() | |
Our Lady of Medjugorje Messages ![]() Find messages Enter words or phrase Random Messages “I am calling you to that love which is loyal and pleasing to God. Little children, love bears everything bitter and difficult for the sake of Jesus who is love. Therefore, dear children, pray that God come to your aid, not however according to your desire, but according to His love.” ( From message, 25 Juni 1988 ![]() | Medjugorje Live Current time in Medjugorje (CET): ![]() ![]() Deep concern & disturbing information: Latest news & articles ![]() 15 Aprili 2017 24 Septemba 2016 5 Aprili 2016 2 Oktoba 2015 Latest videos ![]() 11 Juni 2018 10 Mei 2018 13 Aprili 2018 31 Machi 2018 16 Machi 2018 Most read articles ![]() Most watched videos ![]() Most watched Medjugorje Photos Gallery albums ![]() ![]() Favorite content related to Medjugorje" | |||
Our Lady of Medjugorje Messages Medjugorje Videos Medjugorje News & Articles Medjugorje Web Sites Links Picture & Photo Galleries The Polls | Copyright © 2005-2023 Medjugorje WebSite medjugorje.ws medjugorie.ws medugorje.ws ourlady.eu and content contributors | |||