| | Medjugorje Website Updates
Languages: English, Afrikaans, العربية, Български, Беларуская, Català, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Malti, Nederlands, Norsk, Polski, Português, Română, Русский, Shqip, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Svenska, Tagalog, Tiếng Việt, Українська, زبان_فارسی
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu ili lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na Mungu. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo ninyi, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu huu unaomtamani Mungu ambaye ni upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Wakati huu uwe wakati wa maombi. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu ili aijaze mioyo yenu amani kwa sababu Yeye ni amani. Wanangu, mtafuteni Yesu katika ukimya wa mioyo yenu ili azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji Yesu, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu. ” Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto Yesu mikononi mwake. Yesu alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Wakati huu na uunganishwe na sala kwa ajili ya amani na kwa matendo mema ili kusudi ionekane furaha ya kumngoja Mfalme wa amani mioyoni mwenu, ndani ya familia zenu na katika ulimwengu ambao hauna matumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Pepo za uovu, chuki na wasiwasi huvuma duniani kote kuharibu maisha yote. Kwa hiyo Aliye Juu amenituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya amani na ushirika na Mungu na wanadamu. Ninyi, wanangu, ni mikono yangu iliyopanuliwa: ombeni, mfunge na toeni sadaka kwa ajili ya amani, hazina ambayo kila moyo unatamani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ninawaalika kwenye maombi ya nguvu. Umamboleo unataka kuingia katika mawazo yenu na kuwaibia furaha ya maombi na kukutana na Yesu. Kwa hiyo, wanangu wapendwa, fanyeni upya sala katika familia zenu ili moyo wangu wa kimama ufurahi kama siku za kwanza nilipowachagua ninyi na jibu lilikuwa ni maombi mchana na usiku na mbingu haikunyamaza bali ilitolea kwa mahali hapa neema, amani na baraka kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kwenye maombi kwa moyo. Mioyo yenu, wanangu, igeuzwe kuelekea mbinguni kwa maombi, ili mioyo yenu ipate kuhisi Mungu wa upendo anayewaponya na kuwapenda kwa upendo mkuu. Mimi niko pamoja nanyi kuwaongoza kwenye njia ya uongofu wa moyo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ambao Aliye Juu amenituma niwapende ninyi na kuwaongoza katika njia ya uongofu, toeni sala zenu na sadaka zenu kwa ajili ya wale wote walio mbali na wasiojua upendo wa Mungu. Ninyi, wanangu, muwe mashahidi wa upendo na amani kwa mioyo yote isiyotulia. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Aliye Juu ameniruhusu niwe miongoni mwenu, niwaombee, niwe Mama yenu na kimbilio lenu. Ninawaalika wanangu, mrudieni Mungu na kwenye maombi na Mungu atawabariki kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ninawaalika ninyi mwende katika mazingira ya asili na kusali ili kwamba Aliye Juu Sana aseme na moyo wenu na kwamba muweze kuhisi uwezo wa Roho Mtakatifu kushuhudia upendo ambao Mungu anao kwa kila kiumbe. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ninawaalika ninyi nyote kuwa waletaji wa amani na furaha ya Yesu Mfufuka kwa wale wote walio mbali na maombi ili kwa njia ya maisha yenu, upendo wa Yesu uwabadilishe na kuwa katika maisha mapya, maisha ya wongofu na utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Wakati huu uwe wakati wa sala kwa ajili yenu. ”
Other languages: English, العربية, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
Mwotaji Mirjana Dragićević-Soldo alikuwa na matukio ya kila siku kutoka Juni 24, 1981 hadi Desemba 25, 1982. Katika hafla ya kutokezwa kwake kwa kila siku, akimfunulia siri ya kumi, Bikira alimfunulia kwamba atakuwa na tukio la kila mwaka mnamo Machi 18 na ndivyo ilivyokuwa katika miaka hii yote. Tukio hilo lilianza saa 1.33 jioni na kudumu hadi saa 1.39. “Wanangu wapendwa, ninawaalika mpate kumjua Mwanangu vizuri iwezekanavyo kwa sala na rehema. Ili kwa mioyo safi na iliyo wazi mjifunze kusikiliza. Sikilizeni Mwanangu anachowaambieni ili mpate kuona tena kiroho. Kama watu wamoja wa Mungu, kwa ushirika na Mwanangu, ishuhudieni kweli kwa maisha yenu. Ombeni, wanangu, ili kwamba pamoja na Mwanangu muweze kuleta amani, furaha na upendo kwa ndugu zenu wote. Mimi ni pamoja nanyi na ninawabariki kwa baraka zangu za kimama. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ongokeni na mvae mavazi ya toba na maombi ya kina ya kibinafsi na kwa unyenyekevu mwombe Aliye Juu amani. Katika wakati huu wa neema Shetani anataka kuwapotosha ninyi, nanyi wanangu, mwangalieni Mwanangu na kumfuata kuelekea Kalvari, kwa kujikana na kufunga. Niko pamoja nanyi kwa sababu Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kuelekea furaha ya moyo, katika imani inayokua ndani ya wale wote wanaompenda Mungu zaidi ya vitu vyote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ombeni pamoja nami kwa ajili ya amani maana shetani anataka vita na chuki katika mioyo na mataifa. Kwa hiyo salini na, katika siku zenu, toeni sadaka kwa kufunga na kutubu ili Mungu awape amani. Wakati ujao uko kwenye njia panda kwa sababu mwanadamu wa kisasa hataki Mungu. Kwa hiyo ubinadamu unaelekea kwenye upotevu. Ninyi, wanangu, ni tumaini langu. Ombeni pamoja nami kwamba niliyoyaanza Fatima na hapa yatimie. Ombeni na mshuhudie amani katika mazingira yenu na muwe watu wa amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
| | |