| | Medjugorje Website Updates
Languages: English, Afrikaans, العربية, Български, Беларуская, Català, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Malti, Nederlands, Norsk, Polski, Português, Română, Русский, Shqip, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Svenska, Tagalog, Tiếng Việt, Українська, زبان_فارسی
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! kama mama ninawaalika kutubu. Wakati huu ni kwenu, wanangu, wakati wa ukimya na sala. Kwa hiyo, katika joto la moyo wenu iote chembe ya tumaini na imani na hivyo, ninyi nanyi, wanangu, siku kwa siku mtasikia haja ya kusali zaidi. Maisha yenu yatakuwa ya mpangilio na yenye kuwajibika. Mtaelewa, wanangu, ya kuwa sisi ni wa kupita hapa duniani na ya kuwa mtasikia haja ya kuwa karibu zaidi na Mungu na kwa upendo mtatoa ushuhuda wa mang'amuzi yenu ya kukutana na Mungu, mtakaoushirikisha pamoja na wengine. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombeeni, lakini siwezi kufanya hivyo bila 'Ndiyo' yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, inasikitisha kwamba katikati yenu, wanangu, yapo mashindano mengi, chuki, masilahi yenu wenyewe na ubinafsi. Wanangu, hivi kwa urahisi mnamsahau Mwanangu, maneno Yake na upendo Wake. Imani inazimika katika roho nyingi na mioyo imetekwa na vitu vya ulimwenguni. Lakini moyo wangu wa kimama unajua ya kuwa katikati yenu kuna wale wanaoamini na kupenda, wale ambao wanajaribu kumkaribia Mwanangu zaidi na zaidi, ambao wanamtafuta bila kuchoka na namna hii, wananitafuta hata mimi. Hawa ndio wanyenyekevu na wapole ambao, pamoja na maumivu na mateso wanayoyachukua katika kimya, pamoja na tumaini lao na hasa pamoja na imani yao, ni mitume wa upendo wangu. Wanangu, mitume wa upendo wangu, ninawafundisha ya kuwa Mwanangu hatafuti sala tu pasipo kuchoka bali hata matendo na hisia. Salini ili katika sala mpate kuzidi katika imani na katika upendo. Mpendane wenyewe kwa wenyewe: hilo ndilo analotaka Yeye, hiyo ndiyo ni njia ya uzima wa milele. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu ameleta mwanga kwa ulimwengu huu. Ameuleta kwa wale ambao walitaka kuuona na kuupokea. Hawa muwe ninyi, maana huu ndio mwanga wa ukweli, wa amani na wa upendo. Mimi ninawaongoza kama mama kumwabudu Mwanangu, kumpenda pamoja nami. Fikira zenu, maneno na matendo yenu yamwelekee Mwanangu, yawe katika jina Lake: hapo tu moyo wangu utajazwa. Nawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu ambaye ni Mfalme wa amani. Yeye anawapa amani, basi amani hii isiwe yenu tu, wanangu, lakini wapelekeeni na wengine katika furaha na unyenyekevu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombeeni katika wakati huu wa neema ambayo Mungu anataka kuwapa. Uwepo wangu ni ishara ya upendo, wakati nipo hapa pamoja nanyi niwalinde na kuwaongoza kuelekea umilele. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Українська
Katika tokeo la mwisho la kila siku tarehe 12 Septemba 1998 Bikira Maria alimwambia Yakobo Kolo ya kuwa ataona tokeo mara moja kila mwaka, tarehe 25 Decemba, siku ya Noeli. Hivyo kumekuwa na tokea hata mwaka huu. Tokeo limeanza saa 7 na dakika 38 na likadumu dakika 9. Bikira Maria amekuja pamoja na Mtoto Yesu mikononi mwake. Bikira Maria kwa njia ya Yakobo alipitisha ujumbe huu: “Wanangu wapendwa, katika siku hii ya neema ninawaalika kupenda. Wanangu, Mungu anawapenda kupita kiasi na kwa hiyo wanangu, mmejaa imani, bila kutazama nyuma na bila hofu mwachieni kabisa mioyo yenu ili Mungu aijaze kwa upendo wake. Msiwe na hofu kuamini upendo Wake na rehema Yake maana upendo Wake ni mwenye nguvu kuliko kila udhaifu wenu na hofu. Kwa hiyo, wanangu, mmejaa upendo katika mioyo yenu mwamini Yesu na mseme Ndiyo yenu maana Yeye ni njia ya pekee ya kuwaongoza kwa Baba wa milele. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu, Wakati mnaponijia kama Mama kwa moyo safi na wazi, mjue ya kuwa ninawasikiliza, ninawatia moyo, ninawafariji na hasa ninawaombeeni kwa Mwanangu. Najua ya kuwa mnataka kuwa na imani thabiti na kuionyesha kwa njia inayofaa. Neno analotaka Mwanangu kutoka kwenu ni imani ya kweli, thabiti na kubwa. Hivyo kila njia mnavyoielezea ni ya kufaa. Imani ni fumbo la ajabu tunalohifadhi moyoni. Inakaa baina ya Baba wa Mbinguni na wana wake wote. Hutambulika kwa matunda na kwa upendo ambao sisi tunao kwa viumbe vyote vya Mungu. Enyi mitume wa upendo wangu, wanangu, mtumaini Mwanangu! Saidieni ili wanangu wote wajue upendo wake. Ninyi ni matumaini yangu, ninyi mnaojitahidi kupenda Mwanangu pasipo unafiki. Kwa jina la upendo, kwa wokovu wenu, kulingana na mapenzi ya Baba wa Mbinguni na kwa njia ya Mwanangu, nipo hapa katikati yenu. Mitume wa upendo wangu, kwa njia ya sala na sadaka mioyo yenu iangazwe na upendo na mwanga wa Mwanangu. Mwanga ule na upendo ule uangaze wote wale mnaokutana na uwarudishe kwa Mwanangu! Mimi nipo nanyi. Hasa nipo pamoja na wachungaji wenu: kwa upendo wangu wa kimama ninawaangaza na kuwatia moyo, ili, kwa njia ya mikono iliyobarikiwa na Mwanangu, wabariki ulimwengu mzima. Nawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Wakati huu ndio wakati wa neema na sala, wakati wa kungojea na wa majitoleo. Mungu anajitolea kwenu ili mumpende juu ya kila jambo. Kwa hiyo, wanangu, fumbueni mioyo yenu na jamaa zenu ili kungojea huko kugeuke kuwa sala na upendo na hasa majitoleo. Mimi nipo pamoja nanyi, wanangu, na ninawasihi msiache mema maana matunda yaonekana, yasikika, na yafika mbali. Kwa hiyo adui amekasirika na anafanya kila njia kuwaondoa ninyi katika sala. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu, Moyo wangu wa kimama unateseka wakati ninapotazama wanangu wasiopenda ukweli, wanaouficha; wakati ninapotazama wanangu wasiosali kwa moyo wala kwa matendo. Nimesikitika wakati ninapomwambia Mwanangu ya kuwa wana wangu wengi hawana imani tena, ya kuwa hawamjui Yeye, Mwanangu. Kwa hiyo ninawaalika, mitume wa upendo wangu: mjaribu kutazama mpaka ndani ya mioyo ya watu, na kule bila shaka mtapata hazina ndogo iliyofichwa. Kutazama hivyo ni rehema ya Baba wa mbinguni. Kutafuta mema hata palipo maovu makubwa zaidi, kutafuta kuwaelewana wala kutohukumiana: hilo ni neno ambalo Mwanangu anawaombeni. Nami, kama Mama, ninawaalika kumsikiliza. Wanangu, roho ni yenye nguvu kuliko mwili na, ikichukuliwa na upendo na matendo hushinda vikwazo vyote. Msisahau: Mwanangu aliwapendeni na anawapenda. Upendo wake ni pamoja nanyi na ndani yenu, wakati mpo kitu kimoja pamoja naye. Yeye ni mwanga wa ulimwengu, na hakuna mtu wala kitu kiwezacho kumsimamisha katika utukufu wa mwisho. Kwa hiyo, mitume wa upendo wangu, msiwe na hofu ya kushuhudia ukweli! Ushuhudieni kwa hamu, kwa matendo, kwa upendo, kwa sadaka yenu, lakini hasa kwa unyenyekevu. Shuhudieni ukweli kwa wale ambao hawajajua Mwanangu. Mimi nitakuwa karibu nanyi, mimi nitawatia moyo. Shuhudieni upendo usioishi tena, maana huja kutoka Baba wa mbinguni ambaye ni wa milele na anawatolea wana wangu wote umilele. Roho wa Mwanangu itakuwa karibu nanyi. Ninawaalika tena, wanangu: muwaombee wachungaji wenu, ombeni ili upendo wa Mwanangu uweze kuwaongoza. Nawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Ninyi mna neema kubwa ya kuitwa kwa maisha mapya kwa njia ya ujumbe ninaowapeni. Wanangu, huu ni wakati wa neema, wakati na wiko kwa wongofu wenu na kwa vizazi vya wakati ujao. Kwa hiyo ninawaalika, wanangu, kusali zaidi na kumfunulia Mwanangu Yesu moyo wenu. Mimi nipo pamoja nanyi, ninawapenda wote na kubariki kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Shqip, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu, ninawaomba kuwa hodari wala kutowayawaya, maana hata mema madogo zaidi, ishara ya upendo mdogo zaidi hushinda maovu yanayoonekana zaidi na zaidi. Wanangu nisikilizeni ili mema yashinde, ili muweze kujua upendo wa Mwanangu ulio furaha mkubwa zaidi kuliko zote. Mikono ya mwanangu inawakumbatia, Yeye, apendaye nafsi, Yeye ambaye amejitolea kwa ajili yenu na kunajitolea sikuzote tena katika Ekaristi, Yeye aliye na maneno ya Uzima wa milele; kujua upendo wake, kufuata hatua zake, maana yake ni kuwa na mali ya kiroho. Huo ni utajiri unaojaza hisia iliyo njema, na unaoona upendo na mema popote. Mitume wa upendo wangu, wanangu, muwe kama mionzi ya jua ambayo kwa joto la upendo wa Mwanangu inawapasha joto wote wale wanaoizunguka. Wanangu, ulimwengu unahitaji mitume wa upendo, ulimwengu unahitaji sala nyingi, lakini sala zinazosaliwa kwa moyo na roho, si kwa midomo tu. Wanangu, muwe na hamu ya utakatifu mkiwa na unyenyekevu unaomwezesha Mwanangu kufanya kazi kwa njia yenu, kama Yeye apendavyo. Wanangu, sala zenu, fikira zenu na matendo yenu, haya yote yawafungulia ama kuwafungia mlango wa Ufalme wa Mbinguni. Mwanangu aliwaonyesha njia na kuwapa tumaini, mimi ninawafariji na kuwapa moyo maana, wanangu, mimi nilijua maumivu, lakini nilikuwa na imani na tumaini, sasa nimepata thawabu ya uzima katika Ufalme wa Mwanangu. Kwa hiyo, nisikilizeni, jipeni moyo, msiwayawaye. Nawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Shqip, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Hata viumbe vinawapa ishara za upendo wake Mungu kwa njia ya matunda vinayowapa. Nanyi, pia kupitia ujio wangu, mmepokea wingi wa zawadi na matunda. Wanangu, kadiri mlivyoitikia mwaliko wangu, Mungu anajua. Mimi ninawaalika: hamkuchelewa, kateni shauri kuwa watakatifu na kwa maisha ya pamoja na Mungu katika neema na katika amani! Mungu atawabariki na kuwapa mara mia zaidi, ikiwa mnamtumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Shqip, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, maneno yangu ni manyofu lakini yamejaa upendo wa kimama na mahangaiko. Wanangu, juu yenu vivuli vya giza na vya udanganyifu vinaenea zaidi na zaidi, mimi ninawaiteni kuelekea mwanga na ukweli, mimi ninawaita kuelekea Mwanangu. Yeye peke yake huweza kugeuza kukata tamaa na maumivu yetu kuwa amani na utulivu, Yeye peke yake huweza kutoa matumaini katika maumivu makali sana. Mwanangu ni uzima wa ulimwengu, kwa kadiri mtakavyomjua, ndivyo mtakavyomkaribia na kumpenda maana Mwanangu ni upendo, na upendo unageuza yote. Yeye hufanya la ajabu hata neno lisilo la maana bila upendo machoni penu. Kwa hiyo nawaambieni tena ya kwamba mnapaswa kupenda sana ikiwa mnatamani kukua kiroho. Najua, enyi mitume wa upendo wangu, kwamba si rahisi sikuzote, lakini, wanangu, hata njia ngumu ni njia zinazoongoza kwenye ukuaji wa kiroho, wa kiimani na kwa Mwanangu. Wanangu, salini, mfikirie Mwanangu, nyakati zote za siku zenu inueni nafsi zenu kwake nami nitakusanya sala zenu kama maua kutoka bustani nzuri kuliko zote na kumpa Mwanangu. Muwe hakika mitume wa upendo wangu, wapeni wote upendo wa Mwanangu, muwe bustani zenye maua mazuri kuliko yote. Kwa njia ya sala saidieni wachungaji wenu ili waweze kuwa baba za kiroho waliojaa upendo kwa watu wote. Nawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Huu ndio wakati wa neema. Wanangu, salini zaidi, semeni kidogo mkamwache Mungu awaongoze katika njia ya kutubu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwapenda kwa upendo wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, kwa upendo wa kimama ninawaalika kuifunua mioyo kwa imani, kuifunua mioyo kwa Mwanangu, ili katika mioyo yenu upendo kwa Mwanangu uimbe. Hakika, kutoka upendo huo tu, amani huingia nafsini. Wanangu, najua kwamba mna wema, najua kwamba mna upendo, upendo wenye rehema. Wanangu wangu wengi, lakini, wana moyo uliofungwa. Wanadhani kuweza kutenda pasipo kumwelekezea mawazo yao Baba wa mbinguni anayeangaza, pasipo kumwelekezea Mwanangu aliye daima pamoja nanyi katika Ekaristi na ataka kuwasikiliza. Wanangu, mbona hamzungumzi naye? Maisha ya kila mmoja wenu ni muhimu na ya thamani, maana ni zawadi ya Baba wa mbinguni kwa umilele. Kwa hiyo msisahau kamwe kumshukuru. Zungumzeni naye! Najua, enyi wanangu, ya kuwa mambo yatakayokuja hayajulikani kwenu lakini, mambo yenu ya mbele yatakapotokea, mtapata majibu yote. Upendo wangu wa kimama unataka muwe tayari. Wanangu, kwa maisha yenu wekeni katika mioyo ya watu mnaokutana hisia za amani, za mema, za upendo na msamaha. Kwa ajili ya sala, sikilizeni yanayowaambieni Mwanangu na tendeni namna hiyo. Ninawaalika tena kuwaombea wachungaji wenu, wale ambao Mwanangu aliwaita. Kumbukeni ya kuwa wanahitaji sala na upendo. Nawashukuru. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Polski, Português, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa! Mungu aliniita ili niwaongozeni kwake, maana Yeye ndiye nguvu yenu. Kwa hiyo ninawaalika kumwomba na kumtegemea, maana Yeye ndiye kimbizo lenu kutoka kila uovu uliokaribu na kupeleka mioyo mbali kutoka neema na furaha mnakoitwa. Wanangu isheni Mbingu hapa duniani ili mkae vizuri na amri za Mungu ziwe mwanga katika njia yenu. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwapenda nyote kwa upendo wa kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
Other languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Mimi ni Mama wa ninyi nyote na kwa hiyo msiogope kwa sababu mimi ninasikia sala zenu, najua kwamba mnanitafuta na kwa hiyo ninamwomba Mwanangu kwa ajili yenu; Mwanangu ambaye yu katika mwuungo pamoja na Baba wa mbinguni na pamoja na Roho Mfariji, Mwanangu anayewaongoza roho katika Ufalme alikotoka, ambao ni Ufalme wa amani na wa mwanga. Wanangu, mmepewa uhuru wa kuchagua, kwa hiyo mimi kama Mama ninawasihi mchague uhuru kwa mema, na kwa moyo safi na mnyofu mnaelewa, ingawa pengine hamwelewi maneno yote, ndani yenu mng'amue ukweli ni nini. Wanangu, msipoteze ukweli na maisha ya kweli kwa kufuata maneno ya uongo. Kwa njia ya maisha ya kweli Ufalme wa mbinguni huingia katika mioyo yenu, ni Ufalme wa upendo, wa amani na wa maelewano. Katika Ufalme ule, wanangu, hautakuwa na ubinafsi wa kuwaondoa kutoka kwa Mwanangu, kutakuwa na upendo na maelewano na jirani yako. Kwa hiyo kumbukeni, ninawaambieni tena, kusali maana yake ni kuwapenda wengine, kumpenda jirani yako, kujitoa kwa ajili yao; pendeni na toeni kwa jina la Mwanangu, hapo Yeye atatenda kazi ndani yenu na kwa ajili yenu. Wanangu, fikirini daima juu ya Mwanangu, mpendeni bila kipimo na hapo mtakuwa na maisha ya kweli, yatakayokuwa ya milele. Nawashukuru enyi Mitume wa upendo wangu! ”
| | |